Kiswahili 18. ‘Nabii kama Musa’…

BISMILA-HIR RAHMA-NIR RAHIM

 

Amani ya Mwenyezi Mungu na iwe juu yako na apate kukuongoza katika maisha yako. Mjadala mwingi umehusisha aya inayopatikana katika Maandiko ya Biblia ambayo ndiyo kichwa cha somo letu leo. Wasomi wengi wanafahamu kuwa aya hii inaonesha mbele hadi kwa Nabii Muhammad anayeheshimiwa!

Taurati Kumbukumbu la Torati 18:15,18 “BWANA, Mungu [Mwenyezi Mungu] wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zake kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye. Mimi [Mwenyezi Mungu] nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.”
Wasomi wenye akili nyingi hutumia sana aya hizo juu na kwa kujiamini wanasema, huyo ni yule Nabii anayeheshimiwa anayetajwa hapa katika ‘Taurati’ Kumbukumbu la Torati katika Maandiko ya Agano la Kale. Kwa mtazamo wa kawaida inaonekana hakika kwamba hilo laweza kuwa la kweli. Hata hivyo, twahitaji kuyachunguza zaidi madai haya. Wako wengi wanaotoa madai kwa sababu yanapendeza, lakini ngoja, je hakuna baadhi ya wasomi wanaodai kwamba Maandiko ya Biblia yamechafuliwa? Wanasema kwamba yamekuwa ya uongo kiasi cha kutoweza kuyaamini. Basi mbona wasomi hao Waislamu wadondoe kutoka katika chanzo wanachojisikia kuwa kimechafuliwa? Hivi wanajuaje kwamba aya zizo hizo wanazodondoa zenyewe hazimo miongoni mwa zile zilizochafuliwa? Yote hayo ni utata mtupu au huonekana hivyo, isipokuwa kama sisi twatafuta yaliyo kweli mbali na yale ya uongo.

005.048 “Na tumekuteremshia Kitabu kwa (ajili ya kubainisha) haki, kinachosadikisha vitabu vilivyokuwa kabla yake, na kuvihukumia (kama haya ndiyo yaliyoharibiwa au ndiyo yaliyosalimika). Basi wahukumu baina yao kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao kwa kuacha haki iliyokufikia. Na kila (umma) katika ninyi (binadamu) tumeujaalia sharia yake na njia yake. Na kama Mwenyezi Mungu angalitaka angekufanyeni kundi moja (la kufuata sharia moja), lakini anataka kukujaribuni kwa hayo aliyokupeni. Basi shindaneni kuyafikilia mambo ya heri. Ninyi nyote marudio yenu ni kwa Mwenyezi Mungu; naye atakwambieni (yote) yale mliyokuwa mkihitilafiana.
Al-Qur’an, 005.048 (Al Maidah [Meza, Meza Iliyoandaliwa]).

Kurani Tukufu inaeleza wazi kabisa ya kwamba Mwenyezi Mungu ateremshaye hayo Maandiko pia ndiye ayalindaye. Mwenyezi Mungu pia atatuonesha sisi yaliyo ya kweli. Alikuwa ameiteremsha Taurati kwa njia ya Musa, Zaburi kwa njia ya Daudi na Injili kwa njia ya Isa Masihi. Awezaje mwanadamu anayekufa kuthibitisha kwamba kile kilichoteremshwa wakati uliopita sasa kimechafuliwa au kimechanganywa na uongo? Na ni nani aliyeko huko ambaye yuko juu ya Mwenyezi Mungu, na ni nani angeweza kufanya jambo kama hilo? Huenda ziko aya nyingi katika Vitabu Vitakatifu ambazo kwa msomaji wa juu juu tu zinaweza kumpotosha. Lakini kwa dua inayotolewa kwa dhati na saumu maneno hayo yanaweza kueleweka. Kumbukeni ya kwamba mambo ya kiroho hutambuliwa kwa mambo ya kiroho.

Injili Mathayo 11:25 “Wakati ule Yesu [Isa Masihi] akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya [Mwenyezi Mungu] uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga [wajifunzao kwa unyenyekevu].”

Tusipokuwa miongoni mwa wajifunzao kwa unyenyekevu na endapo sisi tuna hekima machoni petu wenyewe, basi, tutakosa kuelewa mambo ambayo mbingu inajaribu kutufunulia. Kwa hiyo ni muhimu kwamba tuombe kwa unyenyekevu na tupewe roho ya mwanafunzi aliye tayari kujifunza. Ni nani kati yetu awezaye kumfundisha Mwenyezi Mungu? Nani awezaye kujua mengi kuliko yeye? Tena katika Injili tunaambiwa yafuatayo…
Injili 1 Wakorintho 2:14
“Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.”

Kwa hakika lingekuwa tusi la kutisha kwa Mwenyezi Mungu, ambaye bila shaka lo lote ameteremsha maneno yaliyotangulia kwa ajili ya wanadamu, hata kule kudokeza tu kwamba yeye, Mwenyezi Mungu hawezi kulilinda neno lake katika ukamilifu wake mbali na watu wenye mawazo maovu [ni kufuru]. Je, Mwenyezi Mungu hana nguvu kuliko Majini (malaika walioanguka) au zaidi ya wale walioathiriwa nayo? Basi yatupasa kuwa miongoni mwa wale waaminio na tusiwe na wale wenye mashaka. Kwa maana mwenye mashaka aliyethibitika hivyo hawezi kupokea kitu cho chote kutoka kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa hasara ya kupotea milele.

Kumbukeni Mwenyezi Mungu hashindwi kamwe kutimiza ahadi yake…
Sura 3.009
رَبَّنَا إِنَّكَ جَامِعُ النَّاسِ لِيَوْمٍ لا رَيْبَ فِيهِ إِنَّ اللَّهَ لا يُخْلِفُ الْمِيعَادَ
003.009 “Mola wetu! Wewe ndiwe Mkusanyaji wa watu katika Siku isiyo na shaka ndani yake. Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi.” (Aali Imran [Familia ya Imran])

Mwenyezi Mungu ameahidi kwamba yale anayoyateremsha atayalinda yasiharibiwe.
Sura 15:09
إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ
“Hakika Sisi ndio tulioteremsha mauidha haya, na hakika Sisi ndio tutakaoyalinda (yasiharibiwe).
Al-Qur’an, 015.009 Al Hijr
Wapo wale walio na shaka kuhusu yale aliyoyafunua Mwenyezi Mungu. Hapo ndipo Nabii Muhammad anatuambia sisi kwamba kama tuna shaka, basi tuwaulize wale waliopewa kile Kitabu (Maandiko ya Biblia) kabla yetu. Yunus 10:94

فَإِنْ كُنْتَ فِي شَكٍّ مِمَّا أَنْزَلْنَا إِلَيْكَ فَاسْأَلِ الَّذِينَ يَقْرَءُونَ الْكِتَابَ مِنْ قَبْلِكَ لَقَدْ جَاءَكَ الْحَقُّ مِنْ رَبِّكَ فَلا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ
010.094 “Na kama unayo shaka juu ya hayo tuliyokuteremshia, basi waulize wale wasomao vitabu kabla yako (Mayahudi na Manasara wale waliosilimu). Kwa yakini haki imekwisha kukujia kutoka kwa Mola wako, kwa hiyo usiwe miongoni mwa wanaofanya shaka.
Al-Qur’an, 010.094 (Yunus [Yona])

Leo twataka kuwauliza wale ambao wamekuwa wakikisoma kile Kitabu, yaani, Maandiko ya Biblia, juu ya nani aliyenenwa habari zake katika Taurati Kumbukumbu la Torati 18:18 “Mimi [Mwenyezi Mungu] nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe.”…
Injili Matendo 3:20-22 “[Mwenyezi Mungu] apate kumtuma Kristo Yesu [Isa Masihi], mliyewekewa tangu zamani; ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu [Mwenyezi Mungu] kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu. Kwa maana Musa kweli alisema ya kwamba, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye katika mambo yote atakayonena nanyi.”

Inakuwa wazi kabisa katika Injili, ya kwamba Isa Masihi angetumwa ambaye angekuwa kama nabii Musa. Ilikuwa ikimtaja Isa wala si mtu mwingine.
Twawezaje kuwa na hakika? Kama tu hatukumpata kwa mara yetu ya kwanza, kwa rehema habari hiyo inarudiwa pamoja na maelezo ya nyongeza yanayotuambia mtu huyo ni nani.
Injili Matendo 7:37-38 ‘Musa huyo ndiye aliyewaambia Waisraeli, Bwana Mungu [Mwenyezi Mungu] wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi [Musa]; msikieni yeye. Yeye ndiye [Isa] aliyekuwa katika kanisa [umma wa walioamini] jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye katika mlima wa Sinai, tena pamoja na baba zetu; ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi.
Injili Matendo 7:52 Kwa maneno yanayoeleweka wazi mjumbe yule Stefano aliwaambia Wayahudi wale wa zamani… “Ni yupi katika manabii ambaye baba zenu hawakumwudhi? Nao waliwaua wale waliotabiri habari za kuja kwake yule Mwenye Haki [Isa Masihi]; ambaye ninyi sasa mmekuwa wasaliti wake, mkamwua.”

Inatuambia sisi kwamba mtu huyu ambaye angekuwa kama nabii Musa, angekuwa ni mtu yule yule aliyekuwa pamoja na wale waliotoka Misri na akawa pamoja na wale waliokuwa jangwani wakati sauti ya Mwenyezi Mungu iliposikika kutoka juu ya Mlima Sinai. Alikuwa ni Isa Masihi aliyekuwa pale. Hilo liko dhahiri kabisa katika aya hii. Hakuwa yule Nabii Muhammad Anayeheshimiwa ambaye alikuwa kule jangwani, bali ni Isa Masihi. Basi sasa sisi tunafahamu ya kwamba Isa Masihi ndiye mtu yule aliyetajwa katika aya ya Kumbukumbu la Torati 18:15 & 18 na wala si mtume Muhammad. Kama tukiwa na subira na kuendelea kuuliza tutang’amua kwamba siku zote Maandiko yanajitafsiri au kujifafanua yenyewe.

Alikuwa ni Isa ambaye alipaswa kuwaongoza wale walioamini kutoka utumwani kama alivyofanya nabii Musa. Musa aliwaongoza Waisraeli kutoka utumwani Misri kwenda kwenye uhuru. Walipita jangwani. Musa alistahimili mapambano mengi, wakati mwingine wale waliokuwa wamewekwa huru walitaka kumwua Musa kwa sababu walikosa subira na walikuwa wamechoka. Ndivyo hata Isa Masihi, kwa njia iyo hiyo anawaongoza watu, wale wanaoamini, kutoka katika jangwa la dhambi na giza na kuwaingiza katika uhuru ufurahishao wa ile kweli. Isa anawaongoza watu kwenda katika nchi ile ya ahadi, yaani, mbinguni, kwa njia ambayo karibu inafanana sana na vile Musa alivyofanya kuwaongoza wana wa Israeli kutoka Misri kwenda Kanaani, nchi ile ya ahadi. Sisi hatutazamii kwenda Kanaani ya duniani bali ile ya Mbinguni. Nchi ile ni nzuri ambayo ndani yake amani inatawala milele na ambako wale wanaotamani amani watakuwako. Watu wenye amani waipendao kweli watakuwa kule. Watu wale ambao maisha yao yamebadilishwa na yule Mmoja ambaye amekuwa akiwaongoza njiani wakati wote. Hebu wewe na mimi tuwe miongoni mwa Mutaqeen (Wenye haki) tunapomruhusu yule Nabii aliye kama Musa, Isa Masihi kutuongoza. Mwenyezi Mungu na akuwezeshe kuwa miongoni mwao ndiyo dua yangu inayotolewa kwa unyenyekevu leo hii.

Imenakiliwa kutoka DivineIslam’s Qur’an Viewer software v2.913
Maandiko ya Biblia kutoka King James Version

Kwa maelezo zaidi: www.salahallah.com

“Nabii kama Musa”

…Mwenyezi Mungu havunji miadi…

Sura 3:9
Aali Imran

Mfululizo na. 18