Kiswahili 16. “Jinsi Ayubu alivyopoteza afya yake na utajiri wake”

BISMILA-HIR RAHMA-NIR RAHIM


 

Mafumbo Mawili!
Pengine wewe unakijua kisa cha Ayubu na jinsi alivyokuwa miongoni mwa watu mashuhuri sana wa Mashariki katika zama zile za kale. Lakini alipitia kilele cha kutisha cha ugonjwa na kupoteza utajiri wake pamoja na sehemu kubwa ya familia yake na hatimaye afya yake iliathirika vibaya sana (Sad 41). Ayubu alipata mateso makali sana. Je, ni nani alihusika na hayo? Kupata jibu kwa kisa hiki hutatua mafumbo mawili hasa…
Je, ni nani aliyemletea Ayubu maumivu makali kama yale, huzuni na hasara ile? Mtu mbaya sana kama huyo angewezaje kuumbwa? Kwa somo hili na somo lo lote jingine tunahitaji kutoa dua zetu sana faraghani maana Mwenyezi Mungu kwa kweli atawaongoza na kuwaelekeza wale wamtafutao kwa dhati. Mwenyezi Mungu ambaye mara kwa mara husamehe na amejaa fadhili (Al-Buruj 14) awe karibu nawe mpendwa msomaji.
Je, hivi Mwenyezi Mungu ambaye ni Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na Mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo (Al Fatihah 1) angeweza kumwumba Ibilisi (Shetani)? Je, yule Aliye Mtakatifu, aliye chimbuko la Amani na Ukamilifu, Mkuu kuliko wote, Aliyetukuzwa tena ambaye ni Mlinzi, na Mhifadhi wa Usalama (Al-Hashr 23), angeweza kuumba dhambi na Shetani yule mwovu? Je, yule aliye na majina mazuri sana (Al Aaraf 180) anaweza kujihusisha kuumba kitu kibaya sana kama dhambi na uovu?
Au lilikuwa ni chaguo la Ibilisi alilofanya, ambalo lilimfanya kuwa Shetani yule mwovu, na Mwenyezi Mungu alimruhusu tu kuwa na uhuru wa kuchagua?
Mwenyezi Mungu hahusiki na kuwako kwake dhambi, ila yeye anayo tiba yake. Si mwenyezi Mungu aliyefanya dhambi iweko, hata ingawa wengine wanadhani kwamba Mwenyezi Mungu ambaye ni Mtakatifu, Mwenye haki na aliye safi kabisa angeweza kuumba Uovu! La, hasha, tusiwaze mawazo kama hayo… kitu kama hicho kisingeingia mawazoni mwetu kuwa Mwenyezi Mungu anahusika na kuwako kwa uovu.
Ilivyotokea mwanzoni!
Haya basi, ilitokeaje? Kwa maana wote wanaweza kuona dhahiri ya kwamba kweli kuna ufisadi wa kutisha duniani na uovu kila mahali tuangaliapo. Vitabu Vitakatifu vinatupa ujuzi juu ya jinsi Ibilisi alivyotokea. Katika Taurati inatuambia sisi kwamba toka mwanzo, mtu huyo, ambaye sasa anaitwa Shetani alikuwa na jina la Lusifa (Taurati Isaya 14:12). Lusifa maana yake “Mchukuzi wa Nuru”. Wakati mmoja alikuwa malaika aliyetukuzwa ambaye alikuwa katika mlima wa Mwenyezi Mungu. (Taurati Ezekieli 28:14-15) “Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami [Mwenyezi Mungu] nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto. Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.”
Mwenyezi Mungu alimwumba Lusifa akiwa safi, mtakatifu na kiumbe mzuri sana. Taratibu wakati ulipopita, Lusifa akaanza kujiangalia mwenyewe na kujikweza mwenyewe badala ya Muumbaji. Aliutamani uzuri wake na kujifikiria sana kuliko alivyopaswa kufikiri. Mawazo kama hayo yalimfikisha mahali ambapo huyo Lusifa alitaka kukipindua kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu. (Taurati Isaya 14:12-14) “Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri (Lusifa), mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kuliko vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.”
Hasa hasa yeye alikuwa hapatani kabisa na Isa Masihi aliyekuwa karibu sana na Mwenyezi Mungu (Aali Imran 45). Lusifa yule malaika afunikaye baada ya muda mwingi kupita aliendeleza chuki dhidi ya Isa Masihi, ambayo ilijitokeza katika maasi ya wazi. Lusifa hakuwa katika baraza la wale Watawala Wakuu walipojadili mambo kati yao (Sad 69). Yaonekana ya kwamba wale Watawala Wakuu walikuwa wakiongea juu ya uumbaji wa mwanadamu, na Lusifa hakuwamo katika hilo Baraza Kuu, yeye alikuwa tu ni kiumbe aliyeumbwa. Viumbe walioumbwa hawakuruhusiwa kuingia katika baraza hilo. Ni jambo la kusikitisha lakini ni la kweli, Lusifa Mchukuzi wa Nuru, alizitumia vibaya fadhila takatifu alizopewa na kuzipotoa njia zake kutokana na mawazo yake machafu. Akawa hana furaha pamoja na cheo chake kitukufu alichokuwa nacho karibu na kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu, kisha ubinafsi ukatia mizizi ndani yake.
Hilo likasababisha maasi makubwa kule Mbinguni, Lusifa alipoeleza kutoridhika kwake miongoni mwa malaika wengi. Chuki hiyo na mawazo machafu, vikawa kama ugonjwa unaoogopwa uambukizao, na wengi wa wale waliomsikiliza walichagua kuwa upande wa Lusifa. Nao pia wakawa wamedanganywa na kupotoshwa, kutokana na hila zake Lusifa. Watawala wale Wakuu waliwaeleza wazi malaika kwamba endapo wangesisitiza kuyafuata mawazo hayo potofu ya Lusifa, basi, ingewalazimu kuondoka Mbinguni.
Vita Mbinguni?
Naam, hatimaye pakawa na vita mbinguni! Injili Ufunuo 12:7-9 “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli [Isa Masihi] na malaika zake wakapigana na yule joka [Shetani]; yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa,yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.” Isa Masihi alisema… “Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme.” Injili Luka 10:18. Wakati mmoja alikuwa kiumbe aliyetukuzwa, akichukua nuru baadaye anaanguka. Je, twaweza kuiona picha kama hiyo, Mbinguni mahali pa amani na utulivu sasa panageuka na kuwa mandhari ya vitar?
Shetani alihoji mapenzi matakatifu ya Mwenyezi Mungu, na kazi yake ya kwanza kabisa ilikuwa ni kuivunja sheria ya Mwenyezi Mungu [zile Amri Kumi]. Baadaye akaja kwa Adamu na Hawa katika bustani ya Edeni na kwa njia ya majaribu yake, aliwafanya pia kutoliamini neno lake Mwenyezi Mungu na jambo hilo likawafanya wazivunje amri. Ulikuwa ni mpango wa Shetani kupigana vita na Mungu wa mbinguni na sheria zake Takatifu kule mbinguni na kisha hapa duniani. Mwenyezi Mungu anayo katiba yake na sheria ili kuwatawala wale aliowaumba. Lingekuwa kosa la kutisha kujiunga upande wa Shetani na kukutwa upande mbaya, ukipigana na serikali ya Mbinguni na sheria zake Takatifu na za haki, yaani, zile Amri Kumi.
Baada ya Shetani kutupwa, aliweka makao yake makuu hapa duniani. Anaendelea kudanganya kama alivyofanya kule mbinguni. Ila sasa uwezo wake wa kudanganya ni mkubwa zaidi. Yeye bado yuko nyuma ya uhalifu, vita, chuki, na umwagaji damu tunaouona duniani leo. Anaendelez kupanda mbegu za uovu, uhalifu, na chuki juu ya wanadamu, lakini Mwenyezi Mungu katika rehema zake nyingi na huruma zake, hatuachi bila kutupa msaada wake. Mwenyezi Mungu Bwana wa ile kweli bado anatupa Roho wa Mwenyezi Mungu (Roho Mtakatifu) kuwatia nguvu wale waaminio (An Nahl 102). Leo hii sisi twaweza kudai ahadi isemayo kwamba wote wanaokuja kwa Mwenyezi Mungu kwa njia ya mjumbe wake aliyemteua Isa Masihi wanaweza pia kujazwa na Roho wa Mwenyezi Mungu (Roho Mtakatifu) na kuweza kupambana na adui huyu mwenye hila nyingi (Shetani)… “kwa maana [mimi Mwenyezi Mungu] nitateta (nitapambana) na yeye atetaye nawe…” Taurati Isaya 49:25
Ni nani aliyemsumbua Ayubu kumletea huzuni kubwa?
Sasa ili kulijibu swali letu lile la kwanza kuanzia mwanzo wa mazungumzo yetu haya…nani aliyeleta mateso na uovu katika maisha ya Ayubu? Taurati Ayubu 1:8 “Kisha BWANA akamwuliza Shetani, Je! umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na uelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.” Alikuwa si mwingine zaidi ya yule Shetani,yule aliyeanguka kutoka mbinguni. Kisa hicho kinaendelea…Taurati Ayubu 1:9-21 “Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Je! huyo Ayubu yuamcha BWANA bure? Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako. BWANA akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA. Ilitukia siku moja hao wanawe na binti zake walipokuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa, mjumbe akamfikilia Ayubu na kumwambia, Hao ng’ombe walikuwa wakilima, na punda walikuwa wakilisha karibu nao; mara Waseba wakawashambulia, wakawachukua wakaenda nao; naam, wamewaua watumishi kwa makali ya upanga, nami peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Moto wa Mungu umeanguka kutoka mbinguni na kuwateketeza kondoo, na wale watumishi, na kuwaangamiza; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wakaldayo walifanya vikosi vitatu, wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam, wamewaua wale watumishi kwa makali ya upanga; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wanao na binti zako walikuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa; mara, tazama, upepo wenye nguvu ukatoka pande za jangwani, ukaipiga hiyo nyumba pembe zake nne, nayo ikawaangukia hao vijana, nao wamekufa; na mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. Ndipo Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka na nchi, na kusujudia; akasema, Mimi nalitoka tumboni mwa mama yangu, nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.” Ni Shetani anayewatesa wote wanaochagua kumfuata Mwenyezi Mungu, lakini uwezo wa Shetani una mipaka yake. Hawezi kutugusa zaidi ya vile Mwenyezi Mungu anavyomruhusu. Siku moja inayokuja upesi uwezo wa Shetani utavunjiliwa mbali. Basi wewe sasa unalijua lile fumbo linalohusu Shetani alivyotokea. Hebu na ukae karibu na Mwenyezi Mungu na Wale anaowatuma kwetu sisi…Roho Mtakatifu (Ruh) na Isa Masihi. Mwenyezi Mungu na akujalie Amani yake ya milele.
Aya zinatoka katika Kurani Tukuru tafsiri ya Yusef Ali na kutoka katika Biblia, King James version. Kwa kujifunza zaidi:
www.salahallah.com

“Jinsi Ayubu Alivyopoteza Afya yake na utajiri wake”

Sad 38:41

Mfululizo na.16