Kiswahili 15. “Ibrahimu, Rafiki [Khalil] yake Mwenyezi Mungu”

Share thisBISMILA-HIR RAHMA-NIR RAHIM

 

Assalamu’ alaikum!

Khalil (Msiri) wa Mwenyezi
Mungu!

Mpendwa msomaji, leo ni somo linalochangamsha mioyo yetu. Hebu fikiria tu kule kuitwa “rafiki” [Khalil] yake Mwenyezi Mungu! Je, waweza kupiga picha ya kitu cho chote kilicho cha maana katika ulimwengu huu kuliko hicho? Hakuna cho chote ambacho kingeleta tumaini zaidi kwa mtu kuliko kuitwa “Rafiki yake [Khalil] Mwenyezi Mungu!” Ni heshima ya juu kuliko zote, lakini inamfanya mtu kuwa mnyenyekevu sana, anapomfikiria Muumbaji huyo wa Malimwengu, Yeye azishikiliaye nyota zinazozunguka katika ukanda wake na kuziongoza nyota zisizohesabika katika mzunguko wake. Lakini ambaye anataka kufanya urafiki nasi! Tafadhali soma haya yafuatayo: 004:125

004:125 ‘Na nani aliye bora kwa dini kuliko yule ambaye ameuelekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu, naye ni mwema, na anafuata mila ya Ibrahimu (kuwa Mwislamu kweli kweli). Na Mwenyezi Mungu amemfanya Ibrahimu kuwa kipenzi chake.’ Sura: 004:125 An Nisaa

Katika hivyo Vitabu Vitakatifu vya Maandiko ya Biblia, hisia iyo hiyo inaonekana. Kumbuka kwamba Musa aliteremshiwa Sheria (Taurati). Sura 5:44 “Hakika tuliteremsha Taurati yenye uongozi na nuru…” Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.” Sura: 005:044 Al Maidah
Tafadhali zingatia haya yaliyo katika Taurati (ya Maandiko ya Biblia) iliyoteremshwa kwa Musa. 2 Mambo ya Nyakati 20:7 “Si wewe, Ee Mungu [Allah] wetu, uliyewafukuza wenyeji wa nchi hii mbele ya watu wako Israeli, ukawapa wazao wa Ibrahimu rafiki yako [Khalil] hata milele?’
Ni heshima iliyoje kuwa rafiki wa karibu sana wa Mwenyezi Mungu! Twaweza kujifunza zaidi juu ya jinsi ya kuwa rafiki zake Mwenyezi Mungu katika Injili. Hapa yule Nabii alitupa mauidha haya… Sura 5:46 “Na tukawafuatishia (Mitume hiyo) Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyokuwa kabla yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyomo ndani yake uongozi na nuru na isadikishayo yaliyokuwa kabla yake katika Taurati, na uongozi na mauidha kwa wamchao (wanaomwogopa).” 005:046 Al Maidah. Twaigeukia (Injili) Yakobo 2:23 “Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu [Allah] ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa Rafiki [Khalil] wa Mungu [Allah].”

‘Marafiki Zake’ Wengine wa Mwenyezi Mungu!’
Musa alikuwa ni mtu ambaye alipata majaribu makubwa ya imani katika maisha yake. Hata hivyo, yeye aliendelea kuwa mwaminifu kwa Mwenyezi Mungu. Na Musa alibarikiwa kumwona Mwenyezi Mungu, kumbukumbu zinasema, “uso kwa uso”. Musa pia alikuwa rafiki yake Mwenyezi Mungu. (Taurati) Kutoka 33:11 “Naye BWANA [Allah] akasema na Musa uso kwa uso, kama vile mtu asemavyo na rafiki yake [Khalil]”…
Mtu mwingine aliyekuwa Khalil wa Mwenyezi Mungu alikuwa Danieli, Nabii. Mara tatu [Taurati] inasema kwamba Mbingu zilimwona kuwa yeye ni ‘mtu apendwaye sana’! (Taurati) Danieli 10:11 ‘Akaniambia, Ee Danieli, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo…’ Angalia pia Danieli 9:23, na 10:19.
Kisha tunaye mtu aliyeitwa “Henoko”. (Taurati) Mwanzo 5:24 ‘Henoko akaenda pamoja na Mungu [Allah], naye akatoweka, maana Mungu [Allah] alimtwaa.’ Kwa karibu mno Henoko alitembea na Mwenyezi Mungu hata hatimaye akamtwaa na kwenda naye kwake.

Mtu anakuwaje ‘Rafiki’ (Khalil) ya
Mwenyezi Mungu?
Je, hiyo ni kazi ngumu isiyowezekana? Hasha, vinginevyo hakuna ye yote miongoni mwa familia ya kibinadamu ambaye angepewa cheo kama hicho. Kwa hiyo, yatupasa kujitahidi kuwa miongoni mwa marafiki (Khalil) zake Mwenyezi Mungu. Lakini kwa jinsi gani? Yatupasa tu kuyachunguza maisha ya wale waliotangulia kupata cheo cha ‘Khalil’ au ‘mtu apendwaye sana’.

Twaona ya kwamba Ibrahimu alimtii Mwenyezi Mungu katika maisha yake ya kila siku. Hili halikuwa jambo fulani alilolitenda tu kinadharia. Lilikuwa sehemu ya maana sana katika maisha yake. Lo lote alilosema Mwenyezi Mungu, Ibrahimu hakuliamini tu na kulitii, bali alilitekeleza katika maisha yake. Lilikuwa ni zaidi ya kuamini tu! Liligeuka na kuwa kitendo! (Taurati) Mwanzo sura ya 12. Ibrahimu alipoitwa kuiacha nchi yake, kufunga mizigo na kwenda, aliisikiliza sauti ya Mwenyezi Mungu na Ibrahimu akatii na kuiacha nchi yake. Akatekeleza matakwa ya Mwenyezi Mungu. Haidhuru yalikuwaje, Ibrahimu alimsikiliza Mwenyezi Mungu kwa makini . Hata wakati ule Mwenyezi Mungu alipomtaka kufanya jambo fulani ambalo kwa wanadamu wenzake lilionekana kuwa ni la kipumbavu sana. Hebu fikiria, kuanza kufungasha mizigo yako na rafiki zako waje kwako na kukuuliza, “Ibrahimu, unafanya nini”? Yaelekea kabisa kwamba Ibrahimu alisema maneno kama haya, “Nafungasha kambi langu”. “Waendapi”? Ibrahimu: “Mimi sijui, Mwenyezi Mungu atanionesha njia”. Pengine baadhi ya rafiki zake huenda walimwita Ibrahimu kuwa ni ‘mwenda wazimu’. ‘Kwa nini wewe uwaache watu wa jumuia yako, familia yako na rafiki zako, tena [sikiliza] Ibrahimu, na amana yako’? Hata hivyo, Ibrahimu alitii kwa moyo wake wote, na kutekeleza kwa vitendo. Hivyo ndivyo ipasavyo kuwa kwa upande wetu tukitaka kuwa miongoni mwa ‘Khalil’, yaani, rafiki zake Mwenyezi Mungu wa karibu sana. Kama Mwenyezi Mungu amesema, basi, sharti tuwe tayari siyo kusikiliza tu, bali kutekeleza kwa vitendo yale aliyosema Mwenyezi Mungu na kutekeleza matakwa yake.

Kuna walau mambo mawili ambayo ni lazima yatokee ili mtu apate kuwa ‘Khalil’ au rafiki wa karibu sana wa Mwenyezi Mungu.
Kwanza, lazima utii kamili uwepo na utii ule usio na swali katika kufanya mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Hili ni sharti, mtu ye yote asiyemtii Mwenyezi Mungu, hawezi kuwa rafiki yake wa karibu sana. Mwenyezi Mungu hatamlazimisha mtu ye yote kufanya kinyume cha nia yake.

Sura 002:256 ‘Hakuna kulazimishwa (mtu kuingia) katika dini.’… Sura 002:256 Al Baqarah

Hivyo utii huo kwa Mwenyezi Mungu hauna budi kuwa wa hiari unaotoka moyoni mwa mtu huyo, bila nguvu yo yote kutoka nje kutumika. Utii huu usio na masharti hautolewi tu kwa Mwenyezi Mungu, bali kwa Neno lililoteremshwa chini, hilo ni pamoja na: (Taurati na Injili ya Maandiko ya Biblia), Taurati (Amri Kumi), Manabii, na Isa al-Masih [Kristo Masihi] (yule Neno atokaye kwa Mwenyezi Mungu)! Sura 3:3

003:003 ‘Amekuteremshia Kitabu kwa haki, kinachosadikisha yaliyokuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili. Zamani – ziwe uongozi kwa watu. Na akateremsha vitabu vingine vya kupambanua baina ya haki na batili.’ Sura 003:003 Aali Imran
Tunaona katika Taurati mfano mwingine wa mtu aliyetii Neno lililotoka kwa Mwenyezi Mungu. Jina lake alikuwa Hajiri, yule kijakazi, mke wa pili wa Ibrahimu. Hali ya maisha yake ilipokuwa haivumiliki katika maisha ya nyumbani mwa Ibrahimu, alikimbia kutokana na kunyanyaswa alikofanyiwa na Sarai, mke wa kwanza wa Ibrahimu. Alikimbilia jangwani, na ilikuwa dhahiri kwamba alikuwa akirudi kwao kule Misri. Malaika wa BWANA akakutana naye kule na kumwuliza… (Taurati) Mwanzo 16:8 ‘Akamwambia, Hajiri, wewe mjakazi wa Sarai, unatoka wa;pi, nawe unakwenda wapi? Akanena, Nakimbia mimi kutoka mbele ya bibi yangu Sarai.’ Ndipo Malaika wa BWANA [Allah] alipomwambia arudi kambini kwa Ibrahimu na Sarai, na kunyenyekea chini ya mikono yake. Mwanzo 16:9 ‘Malaika wa BWANA [Allah] akamwambia, Rudi kwa bibi yako, ukanyenyekee chini ya mikono yake.’ Kwa uaminifu akaitii sauti ya yule Malaika wa BWANA [Allah], akarudi na kunyenyekea. Huo ndio mwelekeo unaotupasa kuwa nao. Sharti tuwe tayari kuisikiliza sauti ya Mwenyezi Mungu na kunyenyekea kwa uaminifu kwake katika mambo yote. Swali moja linabaki, je, tutakuwa wakweli? Kutatokea nini endapo amri itokayo kwa Mwenyezi Mungu inakuja kwa njia tusiyotarajia? Je, hivi mimi bado nitabaki kuwa miongoni mwa ‘Mutaqeen’? Ni wenye haki au wacha-Mungu (Mutaqeen) wanaofuata kwa uaminifu anakowaongoza Mwenyezi Mungu. Kumbuka kwamba Mwenyezi Mungu mawazoni mwake anakutakia wewe mambo mema kabisa. Ni kwa ajili ya usalama wetu milele.
Pili, yatupasa kujua mapenzi ya Mwenyezi Mungu ni nini! Twende wapi kutafuta mapenzi ya Mwenyezi Mungu ni nini? Kurani Tukufu yasema: ‘Sema: “Tumemwamini Mwenyezi Mungu, na yale tuliyoteremshiwa na aliyoteremshiwa Ibrahimu na Ismaili na Ishaka na Yakubu na watoto (wake), na yale aliyopewa Musa na Isa na manabii (wengine) kutoka kwa Mola wao. Hatubagui baina yao hata mmoja, na sisi tunanyenyekea Kwake.”’ Sura: 003:-84 Aali Imran
Tunayaona mapenzi yake Mwenyezi Mungu yakiwa yamefunuliwa wazi kabisa katika Injili iliyoteremshwa kwetu kutoka kwa Isa al-Masih (Kristo Masihi). 1 Wathesalonike 4:3 “Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu [Allah], kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati.” Utakaso ni utakatifu kwa Mwenyezi Mungu, utakatifu wa moyo na maisha! Ni kumruhusu Mwenyezi Mungu kuiandika Sheria yake ya Amri Kumi ndani ya mioyo yetu. Angalia jinsi maagizo yanayoeleweka wazi yalivyotolewa kwetu ili tuyafuate: (Taurati) Mhubiri 12:13 “Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu [Allah], nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.” Isa, aliyeteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu alisema: Yohana 15:14 “Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo.” Kwa hiyo tunaona tunalo jukumu na ni wajibu wetu kumtii Mwenyezi Mungu kikamilifu, kushika Amri zake, na kuyatii Maneno yaliyoteremshwa chini kupitia kwa Isa al-Masih, hivyo ndivyo tunavyokuwa rafiki zake Mwenyezi Mungu kama alivyofanya Ibrahimu. Mwenyezi Mungu na akupe wewe Amani yake ya Milele!

Aya zimenukuliwa kutoka DivineIslam’s Qur’an Viewer software v2.913

Mafungu ya Biblia yanatoka katika Toleo la King James (KJV)

Kwa kujifunza zaidi: www.salahallah.com

“Ibrahimu, Khalil wake Mwenyezi Mungu”

Sura 4:125
An Nisaa

Mfululizo na. 015