39. “Upendo wa Mwenyezi Mungu…katika kusamehe dhambi”

Share thisBISMILA-HIR RAHMA-NIR RAHIM

Asalamu Aleikum!
Salamu katika jina la Mwenyezi Mungu atupendaye sisi kwa upendo wa milele. Mpendwa msomaji, Wakristo wengi ambao hawajui wanasema kwamba Mwenyezi Mungu katika Kurani hana upendo, au kwamba kwa shida sana upendo unatajwa katika Uislamu.
Lakini twaikuta aya ya maana sana katika Sura 3:31 Aali Imran

“…Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakughufirieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufira (na) Mwenye Rehema.”

Mimi, kama Mwadventista Msabato, nagundua ya kwamba upendo umetajwa zaidi ya mara hamsini katika Kurani Tukufu na ya kwamba neno hili ‘msamaha’ na maneno yenye maana inayokaribiana sana yatokanayo na neno lilo hilo yanapatikana humo zaidi ya mara mia mbili! Kusema machache tu hilo ni jambo la kushangaza. Somo ninalotaka tulipitie leo ni jinsi upendo wake Mwenyezi Mungu unavyodhihirishwa katika kusamehe dhambi.

Kama tusingekuwa na msamaha wo wote kutoka kwa Mwenyezi Mungu, tungekuwa tumepotea milele. Kurudi mbali kule nyuma katika siku zile za Adamu alipokuwa Peponi, alifanya dhambi na kupoteza njia yake. Kwa vile sisi tu watoto wake Adamu, sisi pia tulipoteza njia na kwa sababu ya dhambi yake sisi tumerithi tabia isiyokuwa na upendo wa kweli na twaweza kutarajia tu mauti ya milele.

“Kwa hiyo kama kwa mtu mmoja [Adamu] dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi.” Injili Warumi 5:12

Walakini, huo si mwisho, Kurani Tukufu inasema “nitawafutia makosa yao.” Sura 3:195 Aali Imran, pamoja na “msamaha mzuri” wa Mwenyezi Mungu. Sura 15:85 Al Hijr. Lakini hivi ni kwa vipi hilo linatekelezwa kwa mwanadamu? Kipeperushi hiki kidogo kitaichunguza kweli hii ya zamani kwa njia mbalimbali mpya.

Kwa ajili ya ahadi hizi sisi tunalo tumaini tuwezalo kulishikilia ambalo wale wasioamini hawanalo. Tungejihesabu wenyewe kuwa tumebarikiwa kuifanya habari hii ijulikane kwa wote wanaotuzunguka. Kurani Tukufu yatuambia sisi kwamba:
“…Tuliwafadhilisha baadhi ya Manabii kuliko wengine (kwa amali zao zilizo bora zaidi kuliko za wenziwao), na Daudi tulimpa Zaburi.” Sura 17:55 Bani Israeli

Katika Zaburi twasoma: “Lakini kwako kuna msamaha, ili Wewe uogopwe.” Zaburi 130:4. Daudi pia alisihi: “Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu, uzifute hatia zangu zote.” Zaburi 51:9

Gharama ya Msamaha!

Kwa wengi, mawazo kidogo tu huelekezwa kwenye gharama aliyolipa Mwenyezi Mungu kwa kutupa sisi msamaha kwa ajili ya dhambi zetu. Kumbuka kwamba mtu anapofanya dhambi na kutenda tendo baya, daima kuna gharama au malipo.

Mtu fulani anapokukosea wewe, kwa mfano, ameiba kitu fulani cha thamani kutoka nyumbani mwako, kama vile Televisheni yenye skrini kubwa, kisha mwizi huyo anakamatwa, mambo kadhaa yaweza kutokea.

Mwizi huyo aweza kusamehewa, kisha wewe unabeba hasara ya Televisheni yako yenye skrini kubwa! Hivyo wewe unapata hasara.
Mwizi huyo aweza kufungwa gerezani, kisha yeye anateseka kwa kupoteza uhuru wake.
Mtu fulani mwingine, kwa wema wa moyo wake, anajitolea kukupa Televisheni badala ya ile ya kwako. Mwizi anaenda zake akiwa huru. Mtu mwingine huyo anapata hasara mwenyewe.

Kumbuka ya kwamba sikuzote msamaha huja na gharama yake, sikuzote mtu fulani analipa. Hilo linapokuja kwenye dhambi zetu, twaweza kuingia gharama na kulipa bei kwa ajili ya dhambi yetu na kupoteza uzima wa milele kama mshahara wake. “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti…” Warumi 6:23

Kesi hiyo ya tatu ndivyo alivyotufanyia sisi Mwenyezi Mungu. Kama tungeteseka kwa ajili ya dhambi zetu, basi, tungepoteza uzima wetu miilele, lakini kwa sababu ya upendo wake Mwenyezi Mungu, yaani, wema wake na rehema zake kwetu, kwa hiari yake amechukua kesi hiyo mwenyewe. Amemtoa mtu mmoja aliyekuwa kifuani pake Mwenyezi Mungu ili alipe gharama ya dhambi zetu. Ametoa uhai wa Mwanawe pekee badala ya ule wetu. Alikuwa ni yule mtu mmoija aliyekuwa karibu sana na Mwenyezi Mungu. Kalimatu wa Mwenyezi Mungu. Sura 3:39; 3:45; 4:171.
“(Kumbukeni) waliposema malaika: ‘Ewe Maryamu! Mwenyezi Mungu anakupa khabari njema za (kumzaa mtoto bila ya mume, bali kwa kutamkwa Neno tu litokalo kwake (la kukwambia ‘Zaa’ ukazaa pasina kuingiliwa). Jina lake ni Mashi Isa, mwana wa Maryamu, mwenye heshima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa waliopelekwa mbele na Mwenyezi Mungu.” Sura 3:45 Aali Imran
Mwenyezi Mungu alionesha pendo lake kwetu sisi … “alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Warumi 5:8

Ndiyo, rafiki zangu wapendwa, jambo hili mara nyingi hatulitilii maanani! Mtu fulani alilazimika kulipa bei kwa ajili ya dhambi yetu! Gharama ya msamaha ilikuwa kubwa, kubwa mno, yaani, mauti!

“Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake, zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.” Injili Warumi 5:10

“Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, ambaye ninyi mlimwua mkimtundika katika mti. Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi.” Injili Matendo 5:30-31

Kwa hiyo gharama ya msamaha wetu ilikuwa mauti … mauti ya Masihi Isa. Kwa njia hii haki ilitimizwa na rehema iliifikia familia ya mwanadamu. Mwanadamu angeweza kwenda zake akiwa huru kwa sharti kwamba atii masharti ya ukombozi. Mwanadamu anahitaji kuamini na kupokea kile alichofanya Mwenyezi Mungu.

“Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.” Injili Waefeso 1:7

Msamaha Waoneshwa Wazi!

Masihi Isa alikuwa karibu sana na Mwenyezi Mungu na kwa wazi kabisa Isa alimwakilisha Mwenyezi Mungu kiasi kwamba yeye asema:
“ Aliyeniona Mimi amemwona Baba.”
Injili Yohana 14:9
Twapata picha nzuri zaidi ya msamaha wake Mwenyezi Mungu tuonapo jinsi Isa alivyowatendea wale waliomtesa walipokuwa wakimsulibisha msalabani ili auawe. Hapo twaona msamaha wenye kina ukioneshwa katika maisha yake Isa na kwa kiwango kikubwa mno kisichowahi kuonekana duniani kabla ya hapo. Kumbuka kwamba Isa ni “chapa ya nafsi yake” Mwenyezi Mungu. Hapa ipo aya iliyo wazi inayoelezea ukaribu wake kwa Mwenyezi Mungu.

“Yeye [Mwana] kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu…” Injili Waebrania 1:3

Askari wale wa Kiroma walipompigilia Isa kwa misumari pale msalabani kutokana na ombi la Wayahudi … ulionekana tu upendo mwingi na unyenyekevu katika moyo wake Isa. Hakuna chuki aliyoionesha na wakati walipokuwa wakifanya kazi ile ya kuogofya, Isa alikuwa akiwaombea, akisema, “Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo.” Na wale askari wakayapigia kura mavazi yake. Injili Luka 23:34
Sala ile ya Isa ya msamaha iliujumuisha ulimwengu mzima. Ye yote atakaye aweza kuwa na amani kwa Mungu na kurithi uzima wa milele. Hakuna kisasi cho chote kilichotamkwa juu ya wale askari, makuhani, au watawala, Isa aliwahurumia kwa ujinga wao na hatia yao. Alitoa tu lile ombi ili wapate msamaha wao.

Wapendwa rafiki zangu, mwaweza kufanya uwezekano uwepo ili sala ile ya Masihi Isa ipate kujibiwa katika maisha yenu. Sala ile inamjumuisha kila mtu aliyewahi kuishi, ilimjumuisha kila mtu kutoka katika familia nzima ya Adamu.
Ni Mwenyezi Mungu aliyemteremsha Isa humu duniani ili kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi na athari yake. Isa alijipatia haki ya kutusamehe sisi na sasa tunasimama katika upendeleo huo mtakatifu wa kurejeshwa mara moja tena Peponi mwa Mungu. Ni upendo na msamaha wa ajabu huo!

Gharama Kubwa ya Msamaha!

Wengine huenda waweza kuonekana kana kwamba wanafikiri lilikuwa jambo dogo tu kwa Baba kumteremsha Isa duniani kulipa adhabu kwa ajili ya dhambi ya mwanadamu.

Ingawa mpango wa wokovu ulikuwa umewekwa muda mrefu kabla ya uumbaji wa dunia hii;… bado lilikuwa ni pambano hata kwa yule Mfalme wa malimwengu kumtoa Mwanawe pekee ili afe kwa ajili ya jamii yenye dhambi. Lo, siri ya ukombozi hiyo! Upendo wa Mungu huo kwa ulimwengu ambao haukumpenda! Katika vilindi visivyo na mwisho, akili za wale wasiokufa, wakitafuta kuifahamu siri ya upendo huo usioweza kufahamika, watashangaa na kumsujudu.

Basi, sisi twaweza kuitikia kwa njia ya toba kwa Mungu na imani kwa Kristo. Hivyo ndivyo wana wa Adamu walioanguka wawezavyo tena kuwa “wana wa Mungu” wa kupanga.

Injili 1 Yohana 3:1-3
“Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu, na ndivyo tulivyo. Sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.”
Mpendwa, rafiki yake Mwenyezi Mungu, leo hii wewe waweza kufanya maamuzi yako kukubali na kuamini ya kuwa Masihi Isa ndiye yule Mmoja aliyeteremshwa katika dunia hii yenye giza kulipa fidia yetu kwa kutoa uhai wake na damu yake. Kukataa toleo hilo la gharama kungekuwa ni tusi dhahiri kwa Mwenyezi Mungu kwa msamaha wake kwako wewe. Leo hii, uweze kuchagua kuwa na amani kupitia kafara hii ya Masihi Isa!

Kwa maelezo zaidi tafadhali ujisikie huru kuwasiliana nasi kwa tovuti hii chini:
www.salahallah.com

“Upendo wa Mwenyezi Mungu…katika kusamehe dhambi”

Sura 3:31
Aali Imran

Mfululizo na.39

38. “Kumgeukia Mwenyezi Mungu kwa Toba ya Kweli”

Share thisBISMILA-HIR RAHMA-NIR RAHIM

Asalamu Aleikum!
Mpendwa rafiki yake Mwenyezi Mungu! Nakuomba upate kulichunguza somo hili ambalo kwa shida sana linaongelewa habari zake. Amani tamu ya Mwenyezi Mungu na Neema yake na iwe pamoja nawe. Kuna ahadi moja katika Kurani Tukufu, inayokuja kwa wale watubuo (Sauti itasema:) “Haya ndiyo mnayoahidiwa, kwa kila aelekeaye (kwa Mwenyezi Mungu), ajilindaye (na maasia). Sura 50:32 QafToba ya kweli ni nini? Nani alazimikaye kutubu? Haya ni baadhi tu ya maswali tunayotaka kuyajibu katika somo hili fupi.

Aina moja ya toba inayo huzuni ndani yake kwa jambo fulani lililotendwa au kusemwa ambalo limeleta huzuni au maumivu kwa mtu mwingine. Inajumuisha sikitiko au maumivu anayojisikia mtu kuhusiana na mwenendo wake uliopita. Mara nyingi toba hii ni matokeo ya hofu ya kuadhibiwa kunakoweza kuja kama matokeo ya matendo ya mtu huyo. Lakini hiyo si toba ya kweli…
Toba ya Kweli
Toba ya kweli ni huzuni inayoingia mpaka ndani au ni kujuta kwa ajili ya dhambi kama chukizo na fedheha kwa Mwenyezi Mungu na huonekana kama ni uvunjaji wa Sheria yake Takatifu ya Amri Kumi. Kwa uweza wake Mwenyezi Mungu, kwa njia ya Roho Mtakatifu, toba hiyo yaweza kuleta badiliko katika maisha. Toba ya kweli ni badiliko la moyo au kuongoka kutoka dhambini na kwenda kwa Mwenyezi Mungu.
Toba ni kuachana kabisa na mazoea yo yote, ukiguswa moyoni kuwa yamemchukiza Mwenyezi Mungu, hata kama tendo hilo limetendwa kwa mtu fulani, lakini bado linaangaliwa kuwa ni chukizo kwa Mwenyezi Mungu. Toba ya kweli sikuzote ndani yake inatamani kuzitii Sheria Takatifu za Mwenyezi Mungu, yaani, zile Amri Kumi.

Injili yatuambia sisi kuwa “Huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; lakini huzuni ya dunia hufanya mauti.” 2 Wakorintho 7:10

Toba ya kweli ni wakati ule mtu, kwa njia ya Roho Mtakatifu au Ruh wa Mwenyezi Mungu, anasadikishwa ya kwamba anawaza au anatenda lile ambalo limesababisha kuzivunja amri zake Mwenyezi Mungu. Aguswapo sana moyoni, ndipo anafanya maamuzi kumfuata Mwenyezi Mungu kikamilifu na tena anaamua kuishi maisha yake yote kwa ajili ya Mungu. Mwenye dhambi anageuka na kuacha maovu yote ayajuayo moyoni mwake na katika maisha yake kwa nguvu anazopewa na Mwenyezi Mungu. Hii ndiyo toba ya kweli.
Nabii Masihi Isa alikuwa na mengi ya kusema juu ya toba. Humu katika Injili imeandikwa: “Yesu aliposikia aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.” Injili Marko 2:17. Inasema wazi sana kwamba Masihi Isa aliwaita wenye dhambi ili watubu. Hii inatuhusu sisi sote, kwa maana wanaume na wanawake wote wanahitaji toba.

Toba ya kweli huleta matengenezo!
Toba ya kweli iliyonenwa katika Kurani Tukufu yahusu kuachana kabisa na maisha ya dhambi na kuishi maisha ya kumcha Mungu. Yohana au Yahaya aliyemtangulia Masihi Isa alihubiri toba inayowatoa watu dhambini. “Akafika nchi yote iliyo karibu na Yordani, akihubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi.” Injili Luka 3:3.
Ulikuwa na nguvu kweli ujumbe ule wa Yohana… “Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia ibrahimu watoto.” Injili Luka 3:8. Masihi Isa alithibitisha tena kuwa alikuja kuwaita wenye dhambi ili watubu. “Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi, wapate kutubu.” Luka 5:32.
“Na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanzia tangu Yerusalemu.” Luka 24:47

Ujumbe huo uliwajia Israeli ya Kale: “Basi, nitawahukumu ninyi, nyumba ya Israeli, kila mmoja kwa kadiri ya njia zake, asema Bwana MUNGU. Rudini [tubuni], mkaghairi, na kuyaacha makosa yenu yote; basi hivyo uovu wenu hautakuwa uharibifu wenu.” Taurati Ezekieli 18:30

Ishara za Toba ya Kweli!
Katika nyakati zile za zamani Taurati inasema juu ya watu wa Ninawi waliogeuka na kuwa waovu kupindukia. Mpaka hapo walikuwa wameziacha njia zake Mwenyezi Mungu hata akawatumia ujumbe kupitia Nabii Yona (Yunus). Njia za uovu wao zilikuwa zimezama chini sana hata Mwenyezi Mungu akafanya ujumbe upelekwe kwao uliowatikisa sana. “Basi neno la BWANA lilimjia Yona, mwana wa Amitai, kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu.” Yona 1:1-2.
Katika kisa kifuatacho angalia ishara maalumu walizofanya watu wale wa Ninawi kuonesha toba yao ya kweli.
“Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, ‘Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa.’ Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga; wakijivika nguo za magunia [maturubai], tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo. Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu. Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, ‘Kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng’ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji; bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilia Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio mkononi mwake. Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili tusiangamizwe? Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.” Yona 3:4-10.
Watu wale wa Ninawi walionesha ishara za kweli za toba kwa kubadilisha maisha yao kwa dhati. Ujumbe wa Yona uliwafanya wamtafute Mungu kwa moyo mnyofu. Kuanzia mtawala mwenye nguvu sana kwenda chini mpaka kwa wanyama wanyonge walikuwa wamevaa maturubai, wakatangaza saumu, na kuketi katika majivu kama ishara ya unyenyekevu wao kwa Mungu.
Wakasisitiziwa kuacha njia zao mbaya na za uovu na kumwomba Mwenyezi Mungu ili awahurumie. Mwenyezi Mungu akazisikia dua zao na kuona toba yao ya kweli na historia yatufunulia kwamba Ninawi, mji ule wa kale, uliepushwa wasiangamizwe kwa miaka mingine 140. Mungu kwa rehema zake atazisikia dua zetu na kuiona toba yetu.

Mwenyezi Mungu Aahidi kutupa Moyo Mpya
“Basi, nitawahukumu ninyi, nyumba ya Israeli, kila mmoja kwa kadiri ya njia zake, asema Bwana MUNGU. Rudini, mkaghairi, na kuyaacha makosa yenu yote; basi hivyo uovu wenu hautakuwa uharibifu wenu. Tupilieni mbali nanyi makosa yenu yote mliyoyakosa; jifanyieni moyo mpya na roho mpya; mbona mnataka kufa, asema Bwana MUNGU; basi ghairini, mkaishi.” Taurati Ezekieli 18:30-32. Wito wa Mwenyezi Mungu wa kutubu ni kwa watu wote wa kila taifa.

“‘Maana nitawatwaa kati ya mataifa, nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe. Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia Roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.”
Taurati Ezekieli 36:24-27

Basi wengine waweza kuuliza hivi, inakuwaje hata mtu aweze kutubu? Je, jambo hilo latokana na yeye mwenyewe? Hapana, kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu. Basi, moyo wa asili wawezaje kujichochea wenyewe hata upate kutubu wakati hauna uwezo wa kufanya hivyo? Ni kitu gani kinachomfikisha mtu kwenye toba? Ni Masihi Isa. Je, anamfikishaje mtu kwenye toba? Kuna njia elfu moja awezazo kuzitumia kufanya hivyo, sisi twahitaji tu kuomba.

Karama ya Mwenyezi Mungu ya Toba!
“Akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama ikiwezekana Mungu awape kutubu na kuijua kweli.” 2 Timotheo 2:25

“Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.” 2 Petro 3:9
“…Wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu…” Warumi 2:4

Ni kweli iliyoje, basi, kwamba ni Neema nyingi ya Mwenyezi Mungu inayotuvuta tupate kutubu. Sisi wenyewe kama binadamu hatujui hata jinsi ya kutubu. Ni dhahiri tunasikia huzuni au hatia ya dhambi, lakini jinsi ya kugeuka, yaani, jinsi ya kugeuka kabisa katika maisha yetu na kwenda mbali na dhambi mioyoni mwetu, hiyo ni kazi ya Mwenyezi Mungu tu. Wengi kwa mwenendo wao wa nje wataepuka maovu na dhambi nyingi, lakini kama moyo ungechunguzwa ingegunduliwa ya kuwa ndani ya mioyo yao bado wanatamani tendo lile ovu. Ndani ya moyo dhambi ile haijaondolewa, bado imo mle, tena inapendwa sana. Kadiri dhambi inavyozidi kupendwa bado inatushikilia sisi mateka. Ni lazima dhambi iondolewe moyoni kabla mtu hajawa huru.

Yatupasa kuomba tupewe karama ya toba ya kweli, naye Mwenyezi Mungu atatupa. Kumbukeni Isa alipokuja duniani, hakuna mtu hata mmoja aliyekwenda zake bila kutimiziwa ombi lake, lakini wote waliponywa, itakuwa hivyo kwetu pia, ombi letu liwalo lote kuhusu kuiponya mioyo yetu yenye dhambi litajibiwa. Laiti kama tungemwomba tu Mwenyezi Mungu katika maisha yetu ya faragha, yeye ayatunzaye malimwengu pamoja na kuliongoza kundi kubwa la nyota ikiwamo na dunia yetu katika mzunguko wake, anao pia muda na shauku kwa kila mmoja wetu leo hii. Hakuna mtu hata mmoja asiyeonwa naye, hakuna aliye mdogo mno hata asiweze kumwona, naye anangoja kutoa Neema yake hata kwa yule aliye mdogo kabisa. Mpendwa rafiki yake Mwenyezi Mungu, tumwombe leo hii atupe karama ya toba, ili maisha yetu yaweze kuoshwa uchafu wa dhambi kwa njia ya Isa. www.salahallah.com

“Kumgeukia Mwenyezi Mungu kwa Toba ya Kweli”

Sura 50:32 Qaf

Mfululizo na.38

37. “Ibrahimu, Imamu wa Mataifa”

Share thisBISMILA-HIR RAHMA-NIR RAHIM

Asalamu Aleikum!

Ibrahimu alikuwa mtu mkuu wa Mwenyezi Mungu. Aliheshimiwa sana na Mungu, tena alichaguliwa kuwa kielelezo au mfano wa kufuatwa na wengine.
Yeye anaitwa “Imamu wa Mataifa” katika Kurani Tukufu. Twatamani kuyachunguza maisha ya mtu huyu mashuhuri aliyechagua kumfuata Mungu huku ukiwapo uwezekano mkubwa kwake wa kufaulu au kushindwa. Inaelezwa katika Kurani Tukufu kwamba baba yake mwenyewe alimpinga na kuna mwelekeo mkubwa sana kwamba ndugu zake wengine walimpinga pia. Kumfuata Mungu bila ya masharti kwa upande wetu kila mara kunakuwa na gharama. Mara nyingi hawatatuelewa vizuri wale watuzungukao na hasa wale wa familia yetu au umma wetu. Mtu fulani anayemfuata Mungu kwa karibu sana ataangaliwa na watu kama mtu wa ajabu, kwa maana kuifuata sauti ya Mungu kwaweza kutuleta katika mgongano na hata wale wa dini yetu.

“Na (kumbukeni khabari hii:) Mola wake alipomfanyia mtihani (Nabii) Ibrahim kwa amri nyingi; naye akazitimiza. Akamwambia: ‘Hakika mimi nitakufanya Kiongozi [Imamu] wa watu (wote).’ (Ibrahim akasema:) ‘Je, na katika kizazi changu pia?’ Akasema: ‘Ndio lakini) ahadi Yangu haitawafikia (waovu) madhalimu wa nafsi zao’; (itawafikia walio wazuri)’.” Sura 2:124 Al Baqarah

Twataka kumwangalia mara nyingine tena huyo “Imamu wa Mataifa”, kuona aliishi miaka mingapi. Tunayo picha itokayo katika Vitabu Vitakatifu Taurati na Injili ioneshavo jinsi Ibrahimu alivyoenenda katika maisha yake. Kutoka katika vyanzo hivi sisi twaweza kupata mtazamo bora kwa nini Mwenyezi Mungu alimwita Imamu, Kiongozi wa wale wamtafutao Mwenyezi Mungu kwa moyo wao wote.

“Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya BWANA, wafanye haki na hukumu, ili kwamba BWANA naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake.” Taurati Mwanzo 18:19
Hata makafiri walioishi wakati wa Ibrahimu walitambua ya kuwa Mungu alikuwa pamoja naye.
“Ikawa wakati ule Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakamwambia Ibrahimu, wakinena, Mungu yu pamoja nawe katika yote unayotenda.” Taurati Mwanzo 21:22

Je! hivi ni dhahiri kwa makafiri wa leo kujua Mungu yu pamoja nawe na yu pamoja nami? Kama makafiri hawawezi kuona hilo, je, ni kwa sababu sisi tunashindwa kuunganika na Mungu itupasavyo?

Kielelezo cha Ibrahimu
Kuna vielelezo mbalimbali katika maisha yake Ibrahimu ambavyo yatupasa kuviangalia na ambavyo sisi tungeviangalia kama mfano kwetu wa kuiga. Ibrahimu alikuwa na mtazamo wa unyenyekevu sana kuhusu yeye mwenyewe…
“Ibrahimu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu.” Taurati Mwanzo 18:27

Taurati yasema hivi juu yake, “…Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu.” Taurati Mwanzo 26:5

Eneo moja ambalo twatamani kuliangalia lilikuwa ni eneo lile la ukarimu wa Ibrahimu. Mtindo wake wa kumrudishia Mwenyezi Mungu utajiri wake. Kama lilivyo jambo hilo hivi leo, kwa mara nyingi sana, matajiri wamekuwa hivyo kwa sababu ya kuhodhi mali, hii ndiyo maana wao ni matajiri, walakini, Ibrahimu hakuhodhi mali kwa ajili yake binafsi. Kwa ukarimu alimrudishia Mungu sehemu ya kumi ya ongezeko la mali yake. Naam, ni jambo lisilosadikika kama lilivyo, huo ndio mfano ambao hautiliwi maanani na waumini. Wanaridhika kutoa asilimia ndogo zaidi, yaani, asilimia 2 au 3 ya mapato yao, wanasema hiyo inatosha, lakini, je, Taurati yasemaje juu ya kiwango ambacho Ibrahimu alimrudishia Mungu. Wakati uliopita Mwenyezi Mungu aliwajulisha watu kupitia wale manabii wa mwanzo kile anachotarajia kupata kutoka kwa watu wake na kile anachotaka sisi tumrudishie yeye. Mfano huo uliowekwa tangu zamani ndio Ibrahimu na wengine waliufuata wakimpa Mungu kwa moyo wa hiari. Huo ndio mfano wetu pia.
“Tena zaka yote ya ng’ombe, au ya kondoo, kila apitaye chini ya fimbo; sehemu ya kumi watakuwa ni watakatifu kwa BWANA.” Mambo ya Walawi 27:32
Hapa kwa lugha isiyoweza kukosewa ambayo hakuna awaye yote awezaye kukosea, yatuambia sisi ya kwamba Bwana alitarajia kupewa “zaka” au “sehemu ya kumi” ambayo ndiyo maana ya “zaka”. Yaendelea kusema hivi katika Taurati:
“Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya BWANA; ni takatifu kwa BWANA.” Mambo ya Walawi 27:30

Tunao ushauri huo uliofuatwa na Ibrahimu muda mrefu kabla ya wakati huu. Kumbukumbu yasema kwamba Ibrahimu alitoa sehemu ya kumi au zaka kwa kuhani wa Mungu, Melkizedeki.

“Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako.” Abramu [Ibrahimu] akampa fungu la kumi la vitu vyote.” Taurati Mwanzo 14:20

Tendo hilo lilikuwa la maana sana ambalo Ibrahimu alilitenda kiasi kwamba liliandikwa tena miaka mingi baadaye katika Injili. “Bali yeye [Melkizedeki]; ambaye uzazi wake haukuhesabiwa kuwa umetoka kwa hao, alitwaa sehemu ya kumi kwa Ibrahimu, akambariki yeye aliye na ile ahadi.”
Injili Waebrania 7:6

Mwenyezi Mungu auliza Swali!
“Je! mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu [sadaka].” Malaki 3:8

Hapo kale watu wake Mwenyezi Mungu walimwibia kwa kukataa kumrudishia zaka au sehemu ya kumi. Waliitumia wenyewe, na kujifanya matajiri, lakini tendo hilo lilifikiriwa kuwa ni kumwibia Mungu.

Jambo hilo lipo hata leo. Mwenyezi Mungu ametupa utajiri wake kwa wingi, naye anataka sisi tumrudishie sehemu ya kumi ya ongezeko tupatalo na juu ya hiyo tutoe sadaka. Hapo kale wale waliokuwa waaminifu katika Israeli walitoa asilimia ishirini au hata zaidi kwa ajili ya kazi ya Mungu. Leo hii sisi kama watu tuishio mwisho wa kufungwa historia ya ulimwengu huu yatupasa kulizingatia hilo kwa makini sana na kuuiga mfano huo. Je, haitupasi kuwa wacha Mungu zaidi na kuwa tayari kutoa kwa moyo kama wao walivyofanya. Kitu cho chote kilicho pungufu ya hicho kwa kweli ni wizi tena ni kuzuia kile ambacho kwa haki ni chake Mwenyezi Mungu.

Maisha ya Ibrahimu yalikuwa ya ukarimu kadiri alivyozidi kujitahidi kuwa katika amani na Mbingu. Roho ya ukarimu ni roho ya mbinguni. Mbingu ina roho ya kutoa, na roho hiyo inajidhihirisha sana ndani ya Masihi Isa katika kafara yake kuu kuliko zote aliyoitoa pale msalabani. Kwa ajili yetu sisi Mwenyezi Mungu alimtoa Mwanawe pekee, na Kristo, alipokwisha toa vyote alivyokuwa navyo akajitoa nafasi yake, ili mwanadamu apate kuokolewa. Kilichotendeka juu ya ule Mlima Moria miaka elfu mbili iliyopita huonesha kwa lugha isiyo na kifani kwamba Mbingu ilitoa kilicho bora kabisa kwa ajili ya wanadamu ili kutukomboa na kutulipia fidia tusikabiliwe na mauti ya milele. Tukio lile kuu, Isa alipotoa uhai wake kwa ajili ya wanadamu wote lingemgusa kila mtoto wa Mwenyezi Mungu kuwa na moyo wa ukarimu. Kwa upande mwingine, roho ya uchoyo ni roho ya Ibilisi au Shetani. Kanuni inayoonekana katika maisha ya wale waipendao dunia hii ni kupata, kupata. Hivyo wao wanatumainia kujipatia furaha na raha, lakini tunda lao walilolipanda linawaletea taabu na mauti. Mpaka hapo Mungu atakapoacha kuwabariki watoto wake ndipo nao watakapofunguliwa vifungo vya kumrudishia sehemu yake anayodai apewe.

Madai ya Mwenyezi Mungu ya zaka yetu au sehemu yetu ya kumi
“Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi.” Malaki 3:10-11

Mwenyezi Mungu anatutaka sisi tumjaribu au tumpime. Ili sisi tuweze kufanya hivyo, ni lazima tumwamini kama yeye asemavyo. Mimi ningependekeza sana kwamba msomaji azithibitishe ahadi hizo za Mwenyezi Mungu kuona kama ni za kweli! Mrudishie zaka au sehemu ya kumi ya ongezeko la mapato yako na kuona kama madirisha yatafunguka au milango ya mbinguni haitafunguka kwa ajili yako! Ahadi ni kwamba hapatakuwa na nafasi ya kutosha kuiweka mibaraka hiyo. Pia yeye anaahidi kuyalinda mali yetu na mashamba yetu yasiharibiwe. Mimi nimekwisha kumjaribu Mwenyezi Mungu katika jambo hilo, nami naweza kusema kweli ya kuwa ninavyo vingi zaidi kuliko niwezavyo kuvibeba! Mibaraka yake inavizidi vile ninavyomrudishia yeye.

“BWANA ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.” Kumbukumbu la Torati 28:8

Wapendwa rafiki zangu, je, mngependa Mwenyezi Mungu aamuru baraka ije juu yenu? Hivi ndivyo isemavyo na hivi ndivyo atakavyofanya kama tutatekeleza masharti… je, hivi mko tayari kutii na kumrudishia sehemu ya kumi? Basi msiogope kumwomba mibaraka ambayo Mwenyezi Mungu ataiamuru ije juu yenu!

Je, rafiki zangu, hazina yenu iko wapi? Masihi Isa anaielezea hivi kanuni hii. “Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.” Injili Mathayo 6:21

Rafiki zangu, sisi tungebarikiwa endapo tungefuata mfano wa Ibrahimu, Imamu wa Mataifa, wa kumrudishia Mwenyezi Mungu sehemu ya kumi ya ongezeko la mapato yetu.

Unabii wa wakati wa mwisho
Tamati yake kuna unabii mwingi wa zamani wa Isaya 60 ambao unawajumuisha Wana wa Mashariki (Islamu ya leo) katika mkao wa siku za mwisho pamoja na uhusiano wao na Mwenyezi Mungu na watu wake wale walio waaminifu wa kile Kitabu. Watu hao wataleta utajiri wao na kumletea utukufu Mwenyezi Mungu na kuufanya usonge mbele ujumbe wa siku ya mwisho kabla dunia hii haijafikia mwisho wake na kabla Isa hajarejea. Mpendwa, rafiki yake Mwenyezi Mungu, anakutaka wewe ufanye sehemu yako katika kazi yake ya mwisho humu duniani. “Wingi wa ngamia utakufunika, ngamia vijana wa Midiani na Efa; wote watakuja kutoka Sheba; wataleta dhahabu na uvumba; na kuzitangaza sifa za BWANA. Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, kondoo waume wa Nebayothi watakutumikia; watapanda juu ya madhabahu yangu kwa kibali, nami nitaitukuza nyumba ya utukufu wangu. Ni nani hawa warukao kama wingu, na kama njiwa waendao madirishani kwao? Hakika yake visiwa vitaningojea, na merikebu za Tarshishi kwanza, ili kuleta wana wako kutoka mbali, na fedha yao na dhahabu yao pamoja nao, kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wako, kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli, kwa kuwa amekutukuza wewe. Na wageni watajenga kuta zako, na wafalme wao watakuhudumu; maana katika ghadhabu yangu nalikupiga, lakini katika upendeleo wangu nimekurehemu.” Taurati Isaya 60:6-10.
www.salahallah.com

“Ibrahimu, Imamu wa Mataifa”

Sura 2:124
Al Baqarah

Mfululizo na.37

36B. “Saa ya Hukumu”

Share thisBISMILA-HIR RAHMA-NIR RAHIM

Asalamu Aleikum!

Mpendwa msomaji, hebu leo hii na iwe juu yako Amani na Huruma itokayo kwa Mwenyezi Mungu, ambaye ni mwingi wa kusamehe na mwingi wa kurehemu! (Sura 2:226 Al Baqarah). Hii ni Sehemu ya Pili ihusuyo somo la Hukumu. .

Katika vyote viwili, yaani, Kurani Tukufu na Vitabu Vitakatifu, somo hili la Saa ya Hukumu mara nyingi linaongelewa juu yake. Kwa kweli, hiyo imetajwa mara 77 katika Kurani Tukufu kama “Siku ya Hukumu” au “Siku ya Kiama” Katika Vitabu Vitakatifu vya Maandiko, tukio hilo mara nyingi linatajwa kama “Siku ya Bwana.” Katika siku hiyo wenye dhambi wote, isipokuwa kama kabla yake walikuwa “wakitubu na kudumu kuamini na kufanya yaliyo mema” (Sura 19:60 Maryam), watapokea ujira wao…”, yaani, “adhabu ya Moto mkali.” Sura 22:4 Al-Hajj.

Maonyo hutangulia Adhabu
Mwenyezi Mungu katika upendo wake na rehema zake ametuambia mapema kabla ya wakati ule, jinsi ya kutoka na kuwa hai na safi katika Hukumu hiyo. Siku zote kabla Mungu hajatuma hukumu zake juu ya mataifa, miji mikubwa au wanadamu, anatuma onyo kuonesha jinsi wawezavyo kuikwepa hukumu hiyo. Watu wakigeuka na kuziacha njia zao mbaya, hukumu inaweza kuahirishwa kwa muda fulani. Lakini kama watu hao wakiendelea tu kuzivunja Sheria Takatifu za Mungu, hukumu hiyo hatimaye huwaangukia. Tunaikuta mifano yake wakati Mwenyezi Mungu alipomtuma Yona (Yunus) kwenda kwenye mji mkubwa wa kale uliojaa maovu wa Ninawi, “Basi neno la BWANA lilimjia Yona, mwana wa Amitai, kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu.”
Mwenyezi Mungu pia alimtuma Nuhu kipindi kirefu kabla ya wakati huo kuwaonya wakazi wa dunia juu ya gharika iliyokuwa ikija. Nuhu aliagizwa kujenga safina ili kuikwepa ile gharika. Mwanzo 6 na 7.

Swali lake Mwenyezi Mungu!
“Mbona mnataka kufa, wewe na watu wako, kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, kama BWANA alivyosema…” Yeremia 27:13

“Tupilieni mbali nanyi makosa yenu yote mliyoyakosa; jifanyieni moyo mpya na roho mpya; mbona mnataka kufa…” Ezekieli 18:31
Haya ndiyo matokeo yatakayotokea twendapo kwa Mungu na kumwomba atupe moyo mpya na roho mpya…

“Ndipo mtazikumbuka njia zenu mbaya, na matendo yenu yasiyokuwa mema, nanyi mtajichukia nafsi zenu kwa macho yenu, kwa sababu ya maovu yenu na machukizo yenu.” Ezekieli 36:31.

Mtaichukia njia yenu ya kwanza ya maisha maovu na mawazo machafu! Mwenyezi Mungu ni wa kushangaza, kama sisi tutamruhusu afanye kazi yake kwa uhuru katika maisha yetu. Hii yote ni sehemu ya utakaso unaoendelea wakati Masihi Isa bado yumo ndani ya Patakatifu pa Mbinguni kule juu. Utakaso wa mioyo yetu na maisha yetu ya dhambi pamoja na matokeo yake yateketezayo.

Hebu na uziangalie ahadi hizi nzito zitokazo kwa Mwenyezi Mungu! Hapo kale Mwenyezi Mungu aliwaambia watu wake…
“Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya, mbona mnataka kufa…?” Ezekieli 33:11

Kuhukumiwa Mbele zake Mwenyezi Mungu
Kuna wakati ambapo dunia yote na wakazi wake wote itawapasa kuhukumiwa mbele zake Mungu. Pale itaonekana iwapo wanastahiki kupokea Uzima wa Milele. Tangazo hilo la hukumu kama hiyo limeandikwa katika kitabu kile cha mwisho cha Ufunuo.
“Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.” Ufunuo 14:6-7

Kutoka katika Kisiwa cha upweke cha Patmo, Yohana au Yahaya, mwandishi wa Ufunuo anaandika kwa wazi:
“Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake;… Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na Kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha Uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.” Injili Ufunuo 20:11-13

Hakuna atakayeikwepa hukumu hiyo
”Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.”
2 Wakorintho 5:10

“Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.” Mhubiri 12:14

Mpango wa Mwenyezi Mungu wa Kukutakasa wewe na Kukuokoa
“Yeye aliye na Mwana, anao huo Uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.” 1 Yohana 5:12

Mpango wa Mwenyezi Mungu ni kukuthibitisha wewe katika Hukumu hiyo. Yupo pale kukushika mkono wako. Hebu na uiangalie aya hii kutoka Isaya. “Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.” Taurati Isaya 1:18

”Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili.” Injili Warumi 8:3

Sasa ni wasaa wetu wa kuziungama dhambi zetu na kuzipeleka mapema hukumuni: “Dhambi za watu wengine zi dhahiri, zatangulia kwenda hukumuni; wengine dhambi zao zawafuata.” 1 Timotheo 5:24
Leo ndio wakati wa kumpokea Masihi Isa kama sadaka yako ya dhambi. Isa anaweza kukuokoa kabisa katika hukumu ile ya mwisho, lakini iwapo tu sisi tumempokea yeye kama Mwokozi wetu binafsi. Shauku ya Mungu ni kuwaokoa wote.

“Ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli. Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake.” 1 Timothewo 2:4-6

Hapa ni picha ya kile atakachofanya Mungu kwa wale wanaompenda! Enyi rafiki zake Mwenyezi Mungu, je! mwampenda?

“Maana nitawatwaa kati ya mataifa, nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe. Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi, nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia Roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda. Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba zenu, nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu. Nami nitawaokoeni na uchafu wenu wote, nitaiita ngano, na kuiongeza, wala sitaweka njaa juu yenu tena.” Ezekieli 36:24-29
Rafiki zangu, je, mnao uchafu? Je, mnayo mambo fulani katika maisha yenu yanayohitaji kutakaswa? Hivi ndivyo anavyojaribu kufanya Mwenyezi Mungu kwa kila mmoja wetu wakati Isa angali bado ndani ya Patakatifu pa Mbinguni. Je, tutamruhusu afanye kazi yake ya kimbingu? Je, tutasema kwake ndiyo daima?

Mwombezi wa Mwanadamu ni Isa
Kwa hiyo ni mpango wa Mwenyezi Mungu kuokoa, je, utafanya kazi pamoja naye ili akuokoe? Je, utamruhusu akuokoe kwa njia yake aliyoichagua yeye?
“Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.” Matendo 4:12

Jina hilo linalostahiki si jingine ila ni lake Masihi Isa, Mwokozi wa wanadamu wote. Je, utampokea katika maisha yako?

Zamani sana ilitabiriwa na Mwenyezi Mungu kupitia manabii wale wa kale, ya kwamba Mwenyezi Mungu angemteremsha Mmoja ambaye angeweza kumhesabia haki mwenye dhambi.

“Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao.” Isaya 53:11

Siku ya Upatanisho

Hapo kale hiyo iliitwa Siku Kuu ya Upatanisho. Siku hiyo Israeli wote walitakiwa kukusanyika mbele zake Mwenyezi Mungu. Siku hiyo, siku iliyoitwa kila mwaka kuwa ni “siku ya upatanisho,” Israeli wote walihusika kiakili na kiroho kuzitupilia mbali dhambi zote maishani mwao. Hii ndiyo ahadi aliyotoa Mwenyezi Mungu kwa Israeli ya Kale katika siku ile ya aina yake.

Taurati Mambo ya Walawi 16:30 “Kwa maana siku hiyo upatanisho utafanywa kwa ajili yenu, ili kuwatakasa; nanyi mtatakaswa na dhambi zenu zote mbele za BWANA.”

Tukio hilo la kila mwaka lilihusiana na patakatifu pale pa mfano jangwani, pale pangekuwa kivuli cha tukio kubwa zaidi mwishoni mwa wakati. Tukio hilo la kale lilikuwa kivuli cha tukio ambalo tunaishi nalo sasa. Ni katika wakati huu ambapo Mwenyezi Mungu anapaswa kufanya jambo fulani la pekee. Anataka kuwatenga kabisa watu wake mbali na dhambi zao. Huko ni kutakaswa na dhambi ambako bado hatujawahi kukuona hapa duniani. Je, wewe na mimi tutakuwa na sehemu katika kutakaswa huko kunakofanyika mbinguni?

Amani tamu ya Mbinguni na iwe juu yako.

Aya zimenukuliwa kutoka DivineIslam’s Qur’an Viewer software v2.913

Kwa maelezo zaidi: www.salahallah.com

Isa atakuwa alama ya kukaribia kwa…

“Saa ya Hukumu!”

Sura 43:61
Az-Zukhruf
Sehemu ya Pili

Mfululizo na.36B

36A. “Saa ya Hukumu”

Share thisBISMILA-HIR RAHMA-NIR RAHIM

Asalamu Aleikum!
Wengi sana wamesikia na wanajua habari ya siku ile kuu ya Hukumu. Ni mara ngapi Maimamu wamejadiliana juu ya somo hili na kulisimulia kutoka katika Kurani Tukufu! Ni lini siku hiyo itakuwa imekaribia, je! sisi twaweza kujua? Je, tunajiandaaje kwa siku hiyo ya Hukumu? Je, twaweza kwa njia yo yote ile kuikwepa hiyo hukumu ya mwisho itakapokatwa na mahakama ile?

Wapendwa rafiki zake Mwenyezi Mungu, haya ni maswali machache tu tunayotarajia kuyajadili katika kipeperushi hiki. Mwenyezi Mungu na atupe neema, hekima, na amani ili tupate kulifahamu somo hili. Kurani Tukufu kwa wazi inasema juu ya Saa ya Hukumu.
“Na kwa kweli (Yeye Nabii Isa) ni alama ya Kiama (kuwa kinaanza kutukaribia); msikifanyie shaka na nifuateni. Hii ndiyo njia iliyonyoka.”
Sura 43:61 Az-Zukhruf
Awamu ya Upelelezi ya Hukumu
Kile ambacho watu wachache mno wanatambua ni kwamba kuna awamu ya upelelezi ya hiyo Hukumu Kuu. Kile ambacho wengi sana watakiona kuwa ni cha kushitua mno ni kwamba awamu hiyo ya upelelezi tayari imekwisha anza kwa watu wa dunia hii. Unabii wa zamani uliosahaulika katika Biblia unatuonya mapema ya kwamba siku hiyo tayari imekuja. Iko nyuma yetu zaidi ya vile tunavyodhani sisi kwa sayari hii dunia!

Je, awamu ya upelelezi ya Hukumu hii Kuu ni nini? Katika mahakama yo yote ya kidunia, mtu fulani anaposhitakiwa kuwa ametenda uhalifu fulani, muda unakuwapo mahakama inapokaa, na ushahidi unapoangaliwa kwa makini na kuchunguzwa na mahakama hiyo. Katika hukumu yo yote ya haki kuna kipindi hicho cha upelelezi wa uhalifu uliofanywa, mashahidi huitwa na kuhojiwa na kila jambo huangaliwa kwa makini kabla hukumu ya mwisho haijasomwa na hakimu. Katika kipindi hicho, mahakama inapitia matendo ya mshitakiwa. Jitihada zinafanywa kuona kuwa mambo yote yamekaguliwa kwa makini na kuchunguzwa, ili kujaribu kuona ni makusudi gani yaliyomsukuma mtu huyo kufanya yale aliyofanya.

Katika saa hii tuliyo nayo hivi sasa hapa duniani tumefikia katikati ya sehemu kubwa sana ya hukumu hiyo ya upelelezi inayoendelea. Hii ni kwa kiwango ambacho hakuna cho chote hapa duniani kiwezacho kulinganishwa nayo. Mmojawapo wa unabii wa Biblia wa kipindi kirefu sana katika Danieli 8:14 unatueleza kuhusu tukio hili. Unabii huo ulifikia mwisho wake mwaka 1844, nao wasema “ndipo patakatifu patakapotakaswa”. Unabii huo unaitwa “unabii wa miaka/siku 2300”.
“Akamwambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.” Danieli 8:14
Ni patakatifu gani ambapo Nabii Danieli anaongelea habari zake? Patakatifu hapo au hema hiyo takatifu ni lazima iwe mbinguni. Biblia inazungumza juu ya patakatifu au hema takatifu halisi za aina tatu, ya kwanza iliyotajwa ilikuwa katika siku zile za Musa.
Nabii Musa alikuwa amejenga mfano halisi wa patakatifu pale ambapo alikuwa amepaona akiwa juu ya Mlima pamoja na Mungu. Mfano huo halisi ulijengwa kule nje jangwani baada ya watoto wa Mungu kuondoka Misri. Patakatifu hapo pa jangwani palikuwa mfano halisi mdogo wa pale pa Mbinguni. Kitu fulani ambacho sisi tungeweza kufanya kwa ajili ya watoto wetu, ni kutengeneza mfano halisi wa ndege ambao ungefanana na ndege kubwa.

Musa akiwa juu ya vilele vile virefu vya Mlima Sinai alioneshwa picha ya Patakatifu pa Mbinguni au Hema Takatifu. Kisha aliagizwa na Mungu kujenga mfano halisi mdogo sawa na ule aliokuwa ameoneshwa. Alishauriwa hivi na Mungu…”Nawe angalia ya kwamba uvifanye kama mfano wake, uliooneshwa mlimani.” Taurati Kutoka 25:40

Neno hilo ‘uvifanye’ lilijumuisha Patakatifu pamoja na vitu vyote vinavyohusu samani iliyomo ndani yake. Hivyo vyote vilifunuliwa kwa Musa akiwa juu ya Mlima Sinai.
Kurani Tukufu inalitaja tukio hilo katika aya hii ifuatayo.
“Na (kumbukeni khabari hii kadhalika:) Tulipochukua ahadi yenu (tukakwambieni): ‘Kamateni kwa nguvu haya tuliyokupeni na sikilizeni [sheria].’” Sura 2:93 Al Baqarah
Ni jambo la maana sana kwamba tujifunze somo hili kwa kuwa linafunua jinsi mchakato wa wokovu unavyotekelezwa Mbinguni. Linatupa picha ndogo sana ya kile kinachoendelea kule Mbinguni. Kwa hiyo sisi twaweza kujua ni wakati gani inaanza awamu ya hukumu hiyo ya upelelezi. Unabii wa siku/miaka 2300 ulipokwisha mwaka 1844, Hukumu Kuu ya Upelelezi ilianza kule Mbinguni. Hii ndiyo maana ya kufika muda wa kupatakasa Patakatifu. Patakatifu palipotajwa hapo katika Danieli ni lazima pawe Patakatifu pa Mbinguni, kwa maana patakatifu pale pa jangwani palipojengwa na Musa hatunapo tena na baadaye pakabadilishwa kwa mfano mkubwa zaidi uliojengwa na Sulemani, Mwanawe Daudi. Lakini patakatifu hapo pia hatunapo tena, na paliharibiwa mara mbili. Patakatifu na kutakaswa kwake ambapo pamenenwa katika Danieli ni lazima pawe ni pale pa Mbinguni ambako kiti cha enzi cha Mungu kiko na ambako mahakama inakaa.
“Kiti cha enzi cha utukufu, kilichowekwa juu tangu mwanzo, ndicho mahali patakatifu petu.” Yeremia 17:12. Ni kwa Patakatifu hapo ambapo tunapaswa kutazama kwa utimilifu wa Danieli 8:14.

Pia inataja kwamba patakatifu hapo au hema hiyo takatifu, ya kuwa haikujengwa kwa mikono ya mwanadamu… Injili Waebrania 8:2 “[Isa] Mhudumu wa patakatifu na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu.”
Mwombezi Wetu
Kumbukumbu za wanadamu wote duniani na za matendo yao yote yakiwa mema au mabaya, zimekusanywa na kuwekwa katika Patakatifu pale kule juu. Mahakama inakaa na kupitia maisha yetu na maamuzi hufanywa.

Katika kikao hicho cha mbinguni, Masihi Isa ndiye Mwombezi au Mpatanishi pekee kwa ajili yetu.
“Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu.”
Injili 1 Timotheo 2:5

Ni yeye peke yake anayestahiki kuwa mwombezi wetu, kwa kuwa ni yeye pekee aliyepata haki ya kufanya hivyo kwa kutwaa ubinadamu wetu alipokuja hapa duniani. Yeye bila ubinafsi wo wote alitoa maisha yake juu ya Mlima Moria, ambapo leo hii ipo “Kuba ya Mwamba” au “Msikiti Sharifu” kama kumbukumbu ya daima ya tukio lile la muda mrefu. Hapa pia mapokeo hutuambia kwamba ni mahali pale pale kabisa ambapo Ibrahimu aliitwa na Mungu kumtoa mwanawe kuwa sadaka.
Basi, katika Patakatifu pa Mbinguni Masihi Isa anadai damu yake mwenyewe kuwa inatosha kutukinga. Ni wakati huu wa sasa ambapo sisi hatuna budi kuzingatia hasa kile kinachoendelea kule. Ni wakati huu wa sasa wakati upelelezi huo unapoendelea yatupasa sisi kutafakari kwa makini yale yote ambayo Mungu kwa huruma yake ametufunulia. Wakati umewadia ambao Mungu anafanya mambo haya yajulikane ulimwenguni kote.

Wewe mpendwa msomaji unapendwa sana na Mwenyezi Mungu, upendo wake kwako unapita upendo uwao wote wa kibinadamu. Anakupenda wewe kwa upendo usio na kikomo na kwa shauku kubwa anatamani sana kuiokoa roho yako isiangamizwe milele. Hili ndilo kusudi la kwanza la kipeperushi hiki. Kuna nuru zaidi itakayofunuliwa kwa watu wake Mwenyezi Mungu. Yatupasa kuomba sana tupate kufunuliwa kweli hizi ambazo kwa muda mrefu zimefichwa kwa watu wengi. Leo usikiapo sauti yake ikisema nawe, itika kwake ukisema ndiyo! Kwa bidii mwombe Mwenyezi Mungu katika dua yako ya faragha akufunulie kweli hizi ambazo ni za muhimu kwako kuzijua kwa wakati huu wa Hukumu ya Upelelezi.
Hukumu Yote Amekabidhiwa Mwana
Siyo tu kwamba Isa ni mwombezi, bali twahitaji kufahamu ya kwamba Masihi Isa ndiye aliyeteremshwa kutoka Mbinguni kuwakomboa wote waliomo humu duniani. “[Isa] ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote…”
1 Timotheo 2:6
Ni Masihi Isa yuyu huyu ambaye ameaminiwa na kupewa hukumu ya mwisho ya watu wote.
“Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote; ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba liyempeleka.” Injili Yohana 5:22-23

Ni yale maamuzi ya mwisho, yaliyojengwa juu ya kumbukumbu zilizoko kule mbinguni zihusuzo chaguo letu tulilofanya upande wake au kinyume cha Mungu na kinyume cha yule aliyemteremsha hapa chini kwa ajili yetu, hilo ndilo litaamua matokeo ya hukumu ile itakavyokatwa. Ama tutapewa Uzima wa Milele, ama Mauti ya Milele. Hayo ndiyo malipo yatokanayo na hiyo hukumu. Kipindi hiki tunachoishi sisi ni kipindi cha kuogofya mno. Kingetufanya tupeleke dua zetu za dhati ili tupate kuonekana kuwa hatuna makosa siku ile majina yetu yatakapofikiriwa pale.
Kesi za wote waliomo humu duniani zinaletwa kwenye mahakama ile ya Mbinguni na wote wanachunguzwa kwa karibu sana kana kwamba hawakuwako watu wengine duniani ila wewe tu. Hivyo ndivyo ikatwavyo kwa karibu sana kila kesi.

Masihi Isa na Mahakama ile wanapomaliza kesi hizo, ndipo yeye anakuja duniani akiwa na ujira wake kwa ajili ya Wenye Haki. Waandishi wa kale wa Taurati walitabiri mapema tukio hilo, yaani, wakati atakaporudi na kuja na ujira wake.

“Tazameni,Bwana Mungu atakuja… Tazameni thawabu yake i pamoja naye…”” Taurati Isaya 40:10

Wazo lilo hilo limedhihirishwa katika Ufunuo wa Masihi Isa. Unatabiri waziwazi juu ya wakati ule Isa arudipo kwa ajili ya watu wake waaminifu waliomo duniani, naye analeta thawabu [zawadi] kwa kila mtu aliye mwaminifu.

“Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.” Injili Ufunuo 22:12

Arudipo, kesi za wote zitakuwa zimekwisha katwa. Kwa maana, yeye angewezaje kuja na ujira kama hukumu hiyo ingekuwa bado iko mbele? Rafiki zangu, tunaishi katika Saa Kuu ya Hukumu. Isa arudipo katika mawingu ya Mbinguni, anakuja na ujira wa mwisho. Uzima wa Milele kwa waaminifu na wale wengine wanaangamizwa kwa mng’ao wa kuja kwake.
Tangazo la “Saa ya Hukumu ya Mungu” lilitolewa waziwazi katika miaka ile ya 1843-1844, wakati ujumbe wa pekee wa Ufunuo 14:6 ulipotangazwa waziwazi.

Leo wewe waweza kuwa tayari kwa tukio lile. Tuna Msaidizi wa Mbinguni katika hukumu hii, Masihi Isa; ndiye Mwombezi wako, mlilie yeye.

Kwa maelezo zaidi tafadhali tembelea (tovuti):
www.salahallah.com

Isa atakuwa ishara ya kuja kwa…
“Saa ya Hukumu”

Sura 43:61
Az-Zukhruf
Sehemu ya Kwanza

Mfululizo na.36 A

35. “Divai Safi na Takatifu” -au- “Mvinyo wa Babeli”

Share thisBISMILA-HIR RAHMA-NIR RAHIM

Asalamu Aleikum!

Siku hizi watu wengi wamechanganyikiwa…wamechanganyikiwa kwa kunywa sana vileo ambavyo havikukusudiwa kunywewa na wanadamu. Kwa sababu Ibilisi anazidanganya akili na mioyo ya watu, kwa kileo kilichochachuka, wengi hufanya maamuzi ambayo wasingefanya kama wangekuwa na akili safi. Maelfu huingia katika maangamizi wanapoyatupilia mbali mauidha ya Mwenyezi Mungu. Hakuna ajabu yo yote, mafundisho hayo yanayoeleweka wazi yametolewa katika Kurani Tukufu na katika Vitabu Vitakatifu vya Taurati na Injili ya kuwa divai iliyochachuka au kileo hakipaswi kunywewa kama kinywaji cha mwanadamu. Kwa rehema Mwenyezi Mungu anajaribu kutuonya juu ya hatari hiyo.
“…Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari … katika hivyo mna madhara makuu…” Sura 2:219 Al Baqarah

“…Kunywa mvinyo hakuwafai wafalme; wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo?” Mithali 31:4 Taurati

“…Mola wao atawanywesha kinywaji safi kabisa.” Sura 76:21 Ad-Dahr

Iko divai iliyo safi na takatifu, ni juisi safi ya mizabibu au tunda jinginelo lote. Ni juisi isiyochachuka ya matunda iliyokusudiwa kuwa baraka kwa wanadamu.
“BWANA asema hivi, kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake…” Taurati Isaya 65:8

Ibilisi amemdanganya mwanadamu kutengeneza kileo ambacho kinafanya akili na mioyo ya watu wengi kuchanganyikiwa na kuharibika. Tungekuwa na busara kwa kuyazingatia mauidha yatokayo katika Vitabu Vitakatifu. Masihi Isa alipopewa siki akiwa anapata maumivu makali sana juu ya chombo kile cha kikatili cha kunyongea watu, alipewa siki, lakini alipoionja na kujua ni siki alikataa kuinywa hata katika hali yake ile ya kuteseka.
“Wakampa kunywa divai iliyochanganyika na nyongo; lakini yeye alipoionja hakutaka kunywa.” Injili Mathayo 27:34
Ni kielelezo bora kilichoje hicho ambacho tunacho kutoka kwa Masihi Isa kitufanyacho tukatae cho chote kilichochafuliwa.

Kikombe Hadaa cha Mashetani

Walakini uko mvinyo mwingine, ambao una madhara makubwa zaidi, unafisha, na kuhadaa kuliko mvinyo wenye kileo. Mvinyo huo unaongelewa juu yake katika Vitabu Vitakatirfu vya Biblia, Taurati na Injili. Hakika mvinyo huo umetengenezwa kutoka katika mashamba ya mizabibu ya Shetani mwenyewe, unaitwa “Kikombe cha Mashetani”.
“Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.” 1 Wakorintho 10:20,21

Mvinyo huu ni mchanganyiko wa mafundisho ya kweli na ya uongo au mafundisho potofu ambayo yanafanywa yaonekane kuwa ya kweli . Gilasi nyingi za mvinyo huonekana kuwa safi, mpaka hapo unapouonja. Na, halafu, ukiisha uonja mara nyingi huwa mchungu na mtamu kwa namna inayohatariisha na wapaswa kukataliwa. Mvinyo huo huja ukiwa na ladha inayotia uchungu na kuuma, maana rangi yenyewe tu haiwezi kuudhihirisha mvinyo huo kama ni safi au umechafuliwa. Hivyo ndivyo ilivyo kuhusu mafundisho ya dini. Ni lazima yachunguzwe ili kuona kama mafundisho hayo ni matakatifu au yamechafuliwa. Kwa kila kweli moja ya Mwenyezi Mungu, Ibilisi au Shetani ameweka fundisho lake la uongo na linaonekana kana kwamba ni la kweli , lakini ladha yake ni ya ufisadi na kama mvinyo huo ukinywewa mara nyingi matokeo ni maangamizi.

Twahitaji kuwa na hekima ya kukataa ule uliochafuliwa na kupokea ule ulio safi na mtakatifu. Hivyo ndivyo yalivyo na mafundisho au mafundisho ya dini. Kuna yale yaliyo safi na matakatifu ambayo yanaelekeza kwenye uzima wa milele, kisha yapo yale yaliyochafuliwa na yasiyo safi ambayo huelekeza kwenye maangamizi na kifo.
Ibilisi hunyosha mkono wake ulioshika kikombe cha mashetani kwa kila mmoja wetu kwa njia mbalimbali akijaribu kutushawishi tunywe. Tuna haja ya kuonywa juu ya hila zake. Hili ndilo kusudi la kipeperushi hiki kidogo unachokishika mkononi mwako. Mwenyezi Mungu kwa rehema anamjulisha mtu anayetega sikio lake kusikiliza juu ya utendaji kazi wa siri wa Ibilisi. Upendo wa Mwenyezi Mungu kwa watu ni wa namna ile anayotaka wote wawe macho na kuchukua hadhari dhidi ya hila zake Shetani.

Mvinyo wa Babeli

Mpaka hapa tunataka kuangalia yaliyo ya kweli na yale ya uongo. Taurati na Injili ina mengi ya kusema juu ya mafundisho ya uongo ambayo kwayo Ibilisi amekuwa akiwaongoza mamilioni ya watu. Leo tunataka kuyaweka peupe mafundisho hayo mengi ya uongo na kuyaelezea yale ya kweli kutoka katika Kitabu. Unabii wa kale wa Injili unasema juu ya wakati fulani katika siku hizi za mwisho yatakapopokewa yale ya uongo badala ya yale yaliyo safi.… “Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; na kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti.” Injili 2 Timotheo 4:3

“Lakini wewe nena mafundisho yenye uzima.” Tito 2:1

Kuhusiana na ‘Mvinyo wa Babeli’, inasema: “Kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.” Injili Ufunuo 18:3

Unabii wa Biblia unatuonya kwamba wakuu wa nchi watachafuliwa na huo mvinyo wa uongo uliojaa hadaa. Kwa lugha kuu ya mifano twasoma maneno haya yaliyovuviwa. Kuhusiana na siku hizi za mwisho…”wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao juu ya nchi…” Ufunuo 17:2

Biblia inasema juu ya viongozi wa kitaifa wa dunia walioupokea mvinyo huo au mafundisho ya uongo ya makanisa asi yaliyoanguka, ambayo yako mengi.

Twahitaji kuyaangalia kwa makini mafundisho hayo ya Ibilisi.
Katika Injili twaonywa juu ya nyakati za hatari za siku hizi za mwisho.
“Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepusha nao.” Injili 2 Timotheo 3:1-5
Sasa tunayaanalia mafundisho machache tu kati ya hayo yapotoshayo ambayo yanaitwa ‘Mvinyo wa Babeli’.

1. Mafundisho yameenea sana yasemayo kwamba wale wanaokufa bado wanaweza kuongea na wale walio hai. Lakini Neno la Mungu latwambia kwamba mtu anapokufa anakoma kuwa hai. “Kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.”
Taurati Mhubiri 9:5 Pia Zaburi 146:4

2. Kuchanganya ibada ya sanamu katika ibada yao kwa Mungu kunakubalika kabisa. Walakini hiyo imekatazwa sana na Taurati.
“Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia…” Kutoka 20:4-5

3. Wakristo wengi sana wanamwabudu Maryam. Walakini Neno lasema… “Usiwe na miungu mingine ila Mimi.” Taurati Kutoka 20:3

4. Mamilioni wanadai kwamba Papa wa Roma ni Badala ya au anamwakilisha Kristo. Neno lasema hivi tena, “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu [Ruh wa Mwenyezi Mungu], ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.” Yohana 14:26

5. Makundi kwa makundi ya watu huambiwa kwamba mapokeo ya Kanisa yanaipiku Biblia. “Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu.” Injili Mathayo 15:9. Masihi Isa sikuzote alilitetea Neno la Mwenyezi Mungu, yaani, Biblia, kuwa ndiyo kweli.
”Uwatakase kwa ile kweli; Neno lako ndiyo kweli.” Yohana 17:17. [Aya] hii yaihusu Taurati.

6. Makundi makubwa ya watu wanaungama dhambi zao kwa kasisi, lakini Neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu lasema… “Nalikujulisha dhambi yangu, wala sikuuficha upotovu wangu. Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA , nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.” Zaburi 52:5

7. Vuguvugu kubwa sana la siku za mwisho litakuwa linaitukuza Jumapili kama siku takatifu ya kupumzika iliyotoka kwa Mwenyezi Mungu. Neno la Mungu lasema kwamba Sabato (Jumamosi Siku ya Saba) ndiyo siku ya kupumzika iliyowekwa na Mwenyezi Mungu mwanzoni mwa wakati na ya kwamba sheria zake takatifu ni za haki hazibadiliki.
“Ikumbuke siku ya Sabato [Jumamosi], uitakase.” Taurati Kutoka 20:8. Pia Kumbukumbu la Torati 5:15 na Nehemia 13:22 “Kuitakasa Siku ya Sabato”.

8. Makundi makubwa huambiwa kwamba wokovu waweza kupatikana kwa kutenda matendo mema au kulipa fedha. Neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu lasema tena … “Si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa mara ya pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu.” Injili Tito 3:5

9. Kutoa fedha ili dhambi zako zipate kusamehewa.
“Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.” 1 Petro 1:18,19

10. Msamaha wa dhambi ni kupitia tu Kanisa Katoliki la Roma.
“Ambaye katika yeye [Masihi Isa] tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi.” Wakolosai 1:14

Kwa maelezo zaidi tafadhali tutembelee [tovuti}:
www.salallah.com

“Divai Safi na Takatifu”

-au-

“Mvinyo ya Babeli”

Sura 76:21 Ad-Dahr
Ufunuo 14:8

Mfululizo na..35

34. “Upendo wa Mwenyezi Mungu…katika kusamehe dhambi”

Share thisBISMILA-HIR RAHMA-NIR RAHIM

Asalamu Aleikum!
Salamu katika jina la Mwenyezi Mungu atupendaye sisi kwa upendo wa milele. Mpendwa msomaji, Wakristo wengi ambao hawajui wanasema kwamba Mwenyezi Mungu katika Kurani hana upendo, au kwamba kwa shida sana upendo unatajwa katika Uislamu.
Lakini twaikuta aya ya maana sana katika Sura 3:31 Aali Imran

“…Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakughufirieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufira (na) Mwenye Rehema.”

Mimi, kama Mwadventista Msabato, nagundua ya kwamba upendo umetajwa zaidi ya mara hamsini katika Kurani Tukufu na ya kwamba neno hili ‘msamaha’ na maneno yenye maana inayokaribiana sana yatokanayo na neno lilo hilo yanapatikana humo zaidi ya mara mia mbili! Je, msamaha si kipengele dhahiri cha upendo? Kusema machache tu hilo ni jambo la kushangaza. Somo ninalotaka tulipitie leo ni jinsi upendo wake Mwenyezi Mungu unavyodhihirishwa katika kusamehe dhambi.

Kama tusingekuwa na msamaha wo wote kutoka kwa Mwenyezi Mungu, tungekuwa tumepotea milele. Kurudi mbali kule nyuma katika siku zile za Adamu alipokuwa Peponi, alifanya dhambi na kupoteza njia yake. Kwa vile sisi tu watoto wake Adamu, sisi pia tulipoteza njia na kwa sababu ya dhambi yake sisi tumerithi tabia isiyokuwa na upendo wa kweli na twaweza kutarajia tu mauti ya milele.

“Kwa hiyo kama kwa mtu mmoja [Adamu] dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi.” Injili Warumi 5:12

Walakini, huo si mwisho, Kurani Tukufu inasema “nitawafutia makosa yao.” Sura 3:195 Aali Imran, pamoja na “msamaha mzuri” wa Mwenyezi Mungu. Sura 15:85 Al Hijr. Lakini ni kwa vipi hilo linatekelezwa kwa mwanadamu? Kipeperushi hiki kidogo kitaichunguza kweli hii ya zamani kwa njia mpya mbalimbali.

Kwa ajili ya ahadi hizi sisi tunalo tumaini tuwezalo kulishikilia ambalo wale wasioamini hawanalo. Tungejihesabu wenyewe kuwa tumebarikiwa kuifanya habari hii ijulikane kwa wote wanaotuzunguka. Kurani Tukufu yatuambia sisi kwamba:
“…Tuliwafadhilisha baadhi ya Manabii kuliko wengine (kwa amali zao zilizo bora zaidi kuliko za wenziwao), na Daudi tulimpa Zaburi.” Sura 17:55 Bani Israeli

Katika Zaburi twasoma: “Lakini kwako kuna msamaha, ili Wewe uogopwe.” Zaburi 130:4. Daudi pia alisihi: “Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu, uzifute hatia zangu zote.” Zaburi 51:9

Gharama ya Msamaha!

Kwa wengi, mawazo kidogo tu huelekezwa kwenye gharama aliyolipa Mwenyezi Mungu kwa kutupa sisi msamaha kwa ajili ya dhambi zetu. Kumbuka kwamba mtu anapofanya dhambi na kutenda tendo baya, daima kuna gharama au malipo.

Mtu fulani anapokukosea wewe, kwa mfano, ameiba kitu fulani cha thamani kutoka nyumbani mwako, kama vile Televisheni yenye skrini kubwa, kisha mwizi huyo anakamatwa, mambo kadhaa yaweza kutokea.

Mwizi huyo aweza kusamehewa, kisha wewe unabeba hasara ya Televisheni yako yenye skrini kubwa! Hivyo wewe unapata hasara.
Mwizi huyo aweza kufungwa gerezani, kisha yeye anateseka kwa kupoteza uhuru wake.
Mtu fulani mwingine, kwa wema wa moyo wake, anajitolea kukupa Televisheni badala ya ile ya kwako. Mwizi anaenda zake akiwa huru. Mtu mwingine huyo anapata hasara mwenyewe.

Kumbuka ya kwamba sikuzote msamaha huja na gharama yake, sikuzote mtu fulani analipa. Hilo linapokuja kwenye dhambi zetu, twaweza kuingia gharama na kulipa bei kwa ajili ya dhambi yetu na kupoteza uzima wa milele kama mshahara wake. “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti…” Warumi 6:23

Kesi hiyo ya tatu ndivyo alivyotufanyia sisi Mwenyezi Mungu. Kama tungeteseka kwa ajili ya dhambi zetu, basi, tungepoteza uzima wetu milele, lakini kwa sababu ya upendo wake Mwenyezi Mungu, yaani, wema wake na rehema zake kwetu, kwa hiari yake amechukua kesi hiyo mwenyewe. Amemtoa mtu mmoja aliyekuwa kifuani pake Mwenyezi Mungu ili alipe gharama ya dhambi zetu. Ametoa uhai wa Mwanawe pekee badala ya ule wetu. Alikuwa ni yule mtu mmoja aliyekuwa karibu sana na Mwenyezi Mungu. Aliitwa Neno la Mwenyezi Mungu, Kalimatu wa Mwenyezi Mungu. Sura 3:39; 3:45; 4:171.
“(Kumbukeni) waliposema malaika: ‘Ewe Maryamu! Mwenyezi Mungu anakupa khabari njema za (kumzaa mtoto bila ya mume, bali kwa kutamkwa Neno tu litokalo kwake (la kukwambia ‘Zaa’ ukazaa pasina kuingiliwa). Jina lake ni Masihi Isa, mwana wa Maryamu, mwenye heshima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa waliopelekwa mbele na Mwenyezi Mungu.” Sura 3:45 Aali Imran
Mwenyezi Mungu alionesha pendo lake kwetu sisi … “alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Warumi 5:8

Ndiyo, rafiki zangu wapendwa, jambo hili mara nyingi hatulitilii maanani! Mtu fulani alilazimika kulipa bei kwa ajili ya dhambi yetu! Gharama ya msamaha ilikuwa kubwa, kubwa mno, yaani, mauti!

“Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake, zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.” Injili Warumi 5:10

“Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, ambaye ninyi mlimwua mkimtundika katika mti. Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi.” Injili Matendo 5:30-31

Kwa hiyo gharama ya msamaha wetu ilikuwa mauti … mauti ya Masihi Isa. Kwa njia hii haki ilitimizwa na rehema iliifikia familia ya mwanadamu. Mwanadamu angeweza kwenda zake akiwa huru kwa sharti kwamba atii masharti ya ukombozi. Mwanadamu anahitaji kuamini na kupokea kile alichofanya Mwenyezi Mungu.

“Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.” Injili Waefeso 1:7

Msamaha Waoneshwa Wazi!

Masihi Isa alikuwa karibu sana na Mwenyezi Mungu na kwa wazi kabisa Isa alimwakilisha Mwenyezi Mungu kiasi kwamba yeye asema:
“ Aliyeniona Mimi amemwona Baba.”
Injili Yohana 14:9
Twapata picha nzuri zaidi ya msamaha wake Mwenyezi Mungu tuonapo jinsi Isa alivyowatendea wale waliomtesa walipokuwa wakimsulibisha msalabani ili auawe. Hapo twaona msamaha wenye kina ukioneshwa katika maisha yake Isa na kwa kiwango kikubwa mno kisichowahi kuonekana duniani kabla ya hapo. Kumbuka kwamba Isa ni “chapa ya nafsi yake” Mwenyezi Mungu. Hapa ipo aya iliyo wazi inayoelezea ukaribu wake kwa Mwenyezi Mungu.

“Yeye [Mwana] kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu…” Injili Waebrania 1:3

Askari wale wa Kiroma walipompigilia Isa kwa misumari pale msalabani kutokana na ombi la Wayahudi … ulionekana tu upendo mwingi na unyenyekevu katika moyo wake Isa. Hakuna chuki aliyoionesha na wakati walipokuwa wakifanya kazi ile ya kuogofya, Isa alikuwa akiwaombea, akisema, “Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo.” Na wale askari wakayapigia kura mavazi yake. Injili Luka 23:34
Sala ile ya Isa ya msamaha iliujumuisha ulimwengu mzima. Kwa wote msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia Isa unatolewa bure. Ye yote atakaye aweza kuwa na amani kwa Mungu na kurithi uzima wa milele. Hakuna kisasi cho chote kilichotamkwa juu ya wale askari, makuhani, au watawala, Isa aliwahurumia kwa ujinga wao na hatia yao. Alitoa tu lile ombi ili wapate msamaha wao.

Wapendwa rafiki zangu, mwaweza kufanya uwezekano uwepo ili sala ile ya Masihi Isa ipate kujibiwa katika maisha yenu. Sala ile inamjumuisha kila mtu aliyewahi kuishi, ilimjumuisha kila mtu kutoka katika familia nzima ya Adamu.
Ni Mwenyezi Mungu aliyemteremsha Isa humu duniani ili kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi na athari yake. Isa alijipatia haki ya kutusamehe na sasa sisi tunasimama katika upendeleo huo mtakatifu wa kurejeshwa mara moja tena Peponi mwa Mungu. Ni upendo na msamaha wa ajabu huo!

Gharama Kubwa ya Msamaha!

Wengine huenda waweza kuonekana kana kwamba wanafikiri lilikuwa jambo dogo tu kwa Baba kumteremsha Isa duniani kulipa adhabu kwa ajili ya dhambi ya mwanadamu.

Ingawa mpango wa wokovu ulikuwa umewekwa muda mrefu kabla ya uumbaji wa dunia hii;… bado lilikuwa ni pambano hata kwa yule Mfalme wa malimwengu kumtoa Mwanawe pekee ili afe kwa ajili ya jamii yenye dhambi. Lo, siri ya ukombozi hiyo! Upendo wa Mungu huo kwa ulimwengu ambao haukumpenda! Katika vipindi visivyo na mwisho, akili za wale wasiokufa, wakitafuta kuifahamu siri ya upendo huo usioweza kufahamika, watashangaa na kumsujudu.

Basi, sisi twaweza kuitikia kwa njia ya toba kwa Mungu na imani kwa Kristo. Hivyo ndivyo wana wa Adamu walioanguka wawezavyo tena kuwa “wana wa Mungu” wa kupanga.

Injili 1 Yohana 3:1-3
“Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu, na ndivyo tulivyo. Sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.”
Mpendwa, rafiki yake Mwenyezi Mungu, leo hii wewe waweza kufanya maamuzi yako kukubali na kuamini ya kuwa Masihi Isa ndiye yule Mmoja aliyeteremshwa katika dunia hii yenye giza kulipa fidia yetu kwa kutoa uhai wake na damu yake. Kukataa toleo hilo la gharama kungekuwa ni tusi dhahiri kwa Mwenyezi Mungu kwa msamaha wake kwako wewe. Leo hii, uweze kuchagua kuwa na amani kupitia kafara hii ya Masihi Isa!

Kwa maelezo zaidi tafadhali ujisikie huru kuwasiliana nasi kwa tovuti hii chini:
www.salahallah.com

“Upendo wa Mwenyezi Mungu…katika kusamehe dhambi”

Sura 3:31
Aali Imran

Mfululizo na.34

33. “Nguo za Utawa [Zifunikazo]” sehemu ya pili

Share thisBISMILA-HIR RAHMA-NIR RAHIM

Asalamu Aleikum!
Salamu katika jina lake Mwenyezi Mungu awekaye juu yetu vazi lifunikalo la ‘Haki’. Na ubarikiwe uwe na vazi hilo. Kurani Tukufu yatuambia… “Enyi wanaadamu! Hakika tumekuteremshieni nguo zifichazo tupu zenu na nguo za p ambo, na nguo za utawa (yaani, kucha Mungu) ndizo bora. Hayo ni katika Ishara za (neema za) Mwenyezi Mungu ili wapate kukumbuka.”
Sura 7:026 Al Aaraf
Kurani Tukufu inasema juu ya nguo zifunikazo za aina mbili… ya kwanza ni nguo zifunikazo zilizotengenezwa na wanadamu kuficha aibu yetu na utupu wetu… Hii ndiyo aina moja ya nguo zifunikazo au vazi. Walakini, nguo hizo hazitoshi katika hukumu ile. Kule tunahitaji vazi lifunikalo la aina nyingine lililo bora… Vazi lifunikalo la ‘haki’. Ni kwa vazi pekee lifunikalo la ‘haki’, yaani, hili la pili, ambalo sisi tutapewa, tutaweza kuingia katika ufalme wa Mbinguni.

Kwa nini vazi hili la Haki ni la muhimu sana? Vazi hili la pili lifunikalo linaakisi tabia ya Mungu. Vazi hili la pili ni la mwisho, lakini ni bora. Lilipotezwa katika Bustani ya Edeni wazazi wetu wale wa kwanza walipoanguka kwa kuusikiliza uongo wa Ibilisi. Ili kurudi katika ufalme wa Mungu ambao kutoka katika huo mwanadamu alianguka, anahitaji ‘haki’, ambayo ni kuishi maisha mema na kuwaza mawazo safi, kwa kifupi… “Dini ya Kweli.” Mwenyezi Mungu kwa fadhili zake nyingi alikuwa amempa mtu yule wa kwanza na mkewe uthibitisho mwingi wa wema kwa kumpa yule mume na mkewe mahali kama pale papendezapo katika ile Edeni ya Mungu. Kila mti uliozaa matunda ulikidhi mahitaji yao na yale yote ambayo yangefanya maisha yao kuwa ya furaha na yapendezayo walipewa. Hivyo upendo wa Mwenyezi Mungu ulionekana pande zote ukiwazunguka.
Kwa upande mwingine, Ibilisi alikuwa hajawapa uthibitisho wo wote wa upendo wake kwao wala hakuwapa mahitaji yao, lakini maneno yake yalipokewa upesi na kusadikika kuliko lile Neno la Mwenyezi Mungu. Hivyo ndivyo, mume yule na mkewe waliokuwa watakatifu, walivyoanguka kutoka katika hali yao ya juu walipokula tunda lile lililokatazwa. Wakaipoteza ile haki, yaani, lile vazi zuri lililowafunika walilokuwa wamepewa, walipoacha kumwamini Mungu.

Haki ni kitu fulani kinachotokea ndani ya moyo wa muumini. Tangu anguko lile la mwanadamu, haki ni kitu fulani kisichoweza kutokea kwa juhudi za kibinadamu. Hata wale wasioamini wanaweza kutoa sadaka zao kwa maskini (zakat), na hilo ni jema sana, wanaweza kutenda matendo mengi ya huruma, lakini hayo yaweza kuwa ni mtindo wa haki kwa kuonekana nje na pasiwe na nia halisi kutoka moyoni iwezayo kuwasukuma. Mengi hutendwa kwa madhumuni ya kujionesha kwa watu… ili watu waweze kukusifu kwa wema wako. Hii siyo haki. Hili lilikuwa tatizo huko nyuma katika siku zake Isa [Yesu]. “Tena matendo yao [Wayahudi] yote huyatenda ili kutazamwa na watu…” Injili Mathayo 23:5.

Hata leo hii waumini wanaweza kusema sala zinazorudiwa mara nyingi, ambazo wamezikariri, mara tano kwa siku… walakini hilo linaweza kuwa tendo lifanyikalo bila kufikiri. Ni karibu sana sawa kama mashine… ni kama kumbukumbu iliyorekodiwa, unabonyeza tu swichi, nawe unaisikia sala ile ile… je! hivi hayo ndiyo atakayo Mwenyezi Mungu? Yaani, sala zetu zilizorekodiwa? Bila shaka kuna jambo fulani lenye kina zaidi litakiwalo, pengine sala zetu hazina budi kutoka ndani ya mioyo yetu. Mimi nimebahatika kuwa na watoto na wanapoongea nami kutoka moyoni mwao, naweza kuyathamini sana wasemayo. Waniambiapo kwamba wananipenda, moyo wangu unasisimka. Lakini endapo wangerekodi upendo wao huo kwenye Sidi na kupiga ujumbe huo uliorekodiwa mara nyingi ili nisikilize, moyo wangu usingeguswa hata kidogo. Bila shaka kwa kiasi fulani huenda hilo likafanana na wakati ule tunapomkaribia Mungu. Maongezi yetu pamoja naye ni sharti yatoke ndani yetu na kusemwa kwa moyo wenye shukrani.

Je, hivi kuna jambo fulani litokealo moyoni Mwenyezi Mungu anapotugusa ndani yetu?

Haki ya kweli ni wakati ule matendo mema yatokapo ndani kabisa ya moyo wa mtu. Matendo kama vile… kukataa kulipiza kisasi na kumrudishia mtu fulani anapotukosea. Matendo kama kuwatendea mema maadui zako, kuwa na huruma moyoni mwako… ukikataa kumwumiza mtu fulani aliyekuchukiza sana unapokuwa na uwezo kumdhuru. Kuwa na sala (dua) za faragha kwa ajili ya wale wanaokutesa. Ni Mungu peke yake awezaye kutupa sisi haki ya jinsi hii. Kwa mwanadamu hilo haliwezekani. Ni zawadi kutoka Mbinguni kupitia yule aliyeteremshwa aitwaye Masihi Isa. Tunahitaji watu watakaoomba sana kuwa na utakatifu huu moyoni. Tena yaja ahadi hii kutoka kwa wakuu wale wa Zamani wa Mashariki, ambayo wewe waweza kudai kama yako mwenyhewe.
“Yeye humwomba Mungu, naye akamtakabalia; hata auone uso wake kwa furaha; Naye humrejezea mtu haki yake.”
Ayubu 33:26 Toleo la Kisasa la King James

Mwenyezi Mungu ameahidi kurejeza kile kilichopotea kule Edeni! Enyi rafiki zangu, hizi ni habari njema zenye nguvu… ingawa sisi tumeanguka na kuwa na makosa, bado hatujaachwa. Twaweza kurejezewa tabia ya Mwenyezi Mungu! Yeye ni mwema kwa wasio na shukrani. Anawajali makafiri, akiwapa jua na mvua, vidonda vyao anaviponya… Wasio na shukrani wanacho chakula, mavazi na mahali pa kulala. Mwenyezi Mungu hutoa wokovu kwa wasio haki. Atatufunika tena na vazi lake la Haki. Je, twayasadiki hayo? Hii maana yake ni kuwa na “dini ya kweli” si ule mfano wake tu, bali yenyewe hasa. Kitu fulani cha kweli kitokacho moyoni na kuonekana katika maisha ya kila siku! Hilo likitokea, basi, mfumo wa dua zetu huwa tofauti kabisa. Hatuwi tena na dua zilizorekodiwa ambazo twazisema kwa sauti ya chini na kuharakisha kana kwamba tunatimiza wajibu fulani, lakini itikio litokalo moyoni huonesha Mwenyezi Mungu alivyo wa maana kwetu. Rafiki zangu, je! hayo ndiyo mnayotamani moyoni mwenu? Mwaweza kuwa nayo na yatatolewa kwenu bure! Yote haya hupitia zawadi ya ‘Mwana Mwenye Haki’ aliyeteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Sura 19:10 Maryam.
Hii ndiyo hali ya kila mtu… “Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.” Warumi 7:18
Lakini kama Ibrahimu sisi twaweza kuziamini ahadi… “[Ibrahimu] akamwamini BWANA, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.” Taurati Mwanzo 15:6
Bila kujali kasoro walizo nazo watu wa Mungu, Kristo hawapi kisogo watu wake anaowajali. Anao uwezo wa kuyabadilisha mavazi yao. Anaondoa mavazi machafu [uchoyo wote na dhambi], anaweka juu ya wale wanaotubu na kumwamini vazi lake mwenyewe la Haki, na kuandika msamaha mbele ya majina yao katika kumbukumbu za mbinguni. Anawakiri mbele ya ulimwengu wa mbinguni. Ibilisi, adui yao, anadhihirishwa kuwa ni mshitaki wao na mdanganyaji. Mwenyezi Mungu atatenda haki kwa wateule wake. Mungu wetu asema…
“Mvueni [huyo mwenye dhambi] nguo hizi zenye uchafu. Kisha akamwambia yeye, Tazama, nimekuondolea uovu wako, nami nitakuvika mavazi ya thamani nyingi …” Zekaria 3:4,5.
Hata hivyo, Mungu atakufunika wewe na ”vazi la haki.” Isaya 61:10.

Kumbuka kwamba vazi hili la haki ni ishara itokayo kwa Mwenyezi Mungu… “Na nguo za utawa (yaani kucha Mungu) ndizo bora. Hayo ni katika Ishara za (neema za) Mwenyezi Mungu…” Sura 7:026 Al Aaraf

Hakika vazi hili au kifuniko hiki cha Mwenyezi Mungu ni ile Haki yake Kristo, yaani, tabia yake mwenyewe isiyo na waa, ambalo kwa imani hutolewa kwa wote wanaompokea yeye kama Mwokozi wao kila mmoja binafsi.

Lile vazi jeupe la utakatifu lilivaliwa na wazazi wetu wa kwanza walipowekwa na Mungu katika Edeni takatifu. Waliishi kikamilifu kulingana na mapenzi yake Mungu. Nuru nzuri ambayo mwanga wake ulififia, yaani, nuru ya Mungu iliwazunguka, mume yule na mkewe, ambao walikuwa watakatifu. Vazi hili la nuru lilikuwa ishara ya mavazi yao ya kiroho ya utakatifu wao wenye asili ya mbinguni.. Laiti kama wangalidumu kuwa wanyofu kwa Mungu lingeendelea daima kuwafunika. Walakini dhambi ilipoingia, walikata kiungo chao kilichowaunganisha na Mungu, na ile nuru iliyokuwa imewazunguka ikaondoka. Wakiwa uchi na wakiona aibu, walijaribu kushona majani ya mtini kujifunika ili yawe badala ya mavazi yale ya mbinguni.

Hakuna cho chote awezacho kubuni mwanadamu kiwezacho kuchukua mahali pa vazi lake la utakatifu lililopotea. Ni vazi lile tu lifunikalo ambalo Kristo mwenyewe ametoa laweza kutufanya sisi tufae kuonekana mbele zake Mungu. Vazi hili lifunikalo, yaani, vazi la haki yake, Kristo ataliweka juu ya kila mtu atubuye na kuamini. “Nakupa shauri,” anasema, “ununue kwangu… mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekanwe.” Ufunuo 3:18. Anasema, “ununue”, yaani, litakugharimu kila kitu ili kulipata, lakini lenyewe linatolewa bure.
Vazi hili, lililofumwa katika kiwanda cha mbinguni, ndani yake halina hata uzi mmoja uliobuniwa na mwanadamu. Katika ubinadamu wake Kristo alikuwa na tabia kamilifu, na tabia hii anajitolea kutugawia sisi. “Matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi.” Isaya 64:6
Kila kitu tuwezacho kufanya sisi wenyewe kimechafuliwa na dhambi. Lakini Mwana wa Mungu “alidhihirishwa ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake.” Dhambi inafafanuliwa kuwa ni “uvunjaji wa sheria.” 1 Yohana 3:5,4.
Haki yake Kristo haitafunika dhambi moja inayopendwa sana moyoni.

Ni kile tu kipatanacho na kanuni za sheria ya Mungu kitakachosimama hukumuni.

Hapo baadaye hapatakuwapo na nafasi nyingine ya kujitayarisha kwa umilele. Ni katika maisha haya tunatakiwa kuvaa vazi la haki yake Kristo. Hii ndiyo nafasi pekee kwetu ya kujenga tabia kwa ajili ya makao yale aliyowaandalia wale wanaozishika amri zake. Siku za muda wetu wa kujaribiwa [kupimwa] zinaharakisha sana kuisha. Mwisho ule u karibu. “Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.” Ufunuo 16:15.

Wapendwa rafiki zangu, hatuna muda wa kuchelewa-chelewa na kulipuuzia somo hili muhimu. Sasa ndio wakati wa kusali na kusihi kwa dhati ili Mwenyezi Mungu atupe sisi mbaraka huo. Msifanye kosa, kukosa hapa ni kukosa umilele. Mwenyezi Mungu na atupe ishara yake… yaani, Vazi la Haki.
Kwa maelezo zaidi juu ya somo hili na mengineyo, tafadhali tembelea tovuti yetu chini. Maswali yako au maoni yako yanakaribishwa sana!

www.salallah.com

“Vazi la Haki”
Sehemu ya Pili

Sura 7:26
Al Aaraf

Mfululizo na.33

32. “Nguo za utawa [zifunikazo]” sehemu ya kwanza

Share thisBISMILA-HIR RAHMA-NIR RAHIM

Asalamu Aleikum!
Salamu katika jina lake Mwenyezi Mungu, mwenye rehema nyingi sana na mwenye haki, anayesamehe mara nyingi na mwenye huruma. Roho (Ruh) wa Mwenyezi Mungu awe nanyi mnapolitafakari somo hili ambalo ni la muhimu mno kwetu kulijua!

“Enyi wanadamu! Hakika tumekuteremshieni nguo zifichazo tupu zenu na nguo za pambo, na nguo za utawa (yaani kucha Mungu) ndizo bora.” Hayo ni katika ishara zake (neema za) Mwenyezi Mungu ili wapate kukumbuka.”
Sura 7:026 Al Aaraf

Haki (utawa) bila shaka ni somo la maana, kwa kuwa limetajwa zaidi ya mara 70 katika Kurani Tukufu na zaidi ya mara 200 katika Biblia. Hivi “haki” maana yake nini? Maana iliyo dhahiri ya neno hili ni:
“Usafi wa moyo na uadilifu wa maisha, moyo na maisha yale yanayotii sheria ya Mungu. Haki, kama neno hilo litumikavyo katika Maandiko/Kurani na theolojia, ambamo linatumika sana, linakaribia sana kuwa sawa na utakatifu, yaani, kuzijua kanuni takatifu na mapenzi ya moyo, na maisha yafuatayo sheria ya Mungu. Inajumuisha yote tuyaitayo haki mbele ya sheria, yaani, unyofu wa moyo na wema, kuwa na mapenzi matakatifu, kwa kifupi, hii ndiyo dini ya kweli.”

Basi, twaipataje hiyo “haki”? Je, hivi sisi kwa asili yetu tunayo tabia kama hiyo maishani mwetu?

Adamu na Hawa
Wazazi wetu wale wa kwanza walibarikiwa kwa kuwa na haki katika ile Bustani. Walifanywa kuwa wenye haki, tangu walipoumbwa.…Ilikuwa ni zawadi iliyotoka mbinguni, lakini mara tu walipotenda dhambi waliipoteza zawadi hiyo ya haki. Kwa maneno mengine, walipoyasikiliza madanganyo yake Ibilisi badala ya kulisikiliza Neno la Mwenyezi Mungu wakaanguka kutoka katika haki. Basi, wazao wote wa Adamu hawana njia yo yote ya kuipata tena, isipokuwa kama wakipewa na Mungu. Hatuna wema wo wote katika maisha yetu haya…Wema wetu wote/haki yetu yote ilipotea mwanadamu alipotenda dhambi katika ile bustani. Sisi hatuna haki hiyo kabisa. Wala hatuna wema wo wote ndani ya mioyo yetu, wala hatuwezi kustahili kupata hiyo haki kwa matendo yetu mema.

“Kama ilivyoandikwa, Hakuna mwenye haki hata mmoja.” Injili Warumi 3:10

Kama ilivyoelezwa nyuma katika ile bustani ya Edeni, Adamu na mkewe, wote wawili walikuwa wenye haki. Hawakuwa na haja ya kuwa na nguo zo zote za kujifunika wenyewe, kama ishara ya haki yao walifunikwa na vazi la nuru. Nabii Daudi aliandika hivi:
“Ataitokeza haki yako kama nuru, na hukumu yako kama adhuhuri.”
Zaburi 37:6
Hapo haki ni sawa na Nuru. Hivyo wazazi wetu wale wa kwanza hawakuvaa nguo zo zote zilizotengenezwa na wanadamu, walivikwa nuru. Adamu na Hawa walipoanguka kutoka katika haki, walilipoteza vazi lao lile la mbinguni lililowafunika na, sasa, wakajiona wenyewe kuwa wako uchi na ile nuru hawakuwa nayo kabisa. Walikuwa wameusikiliza uongo wa Ibilisi, na lile vazi la nuru lililowafunika likatoweka. Katika Kurani
Tukufu inaeleza hivi…
“Basi wakaula wote wawili, na uchi wao ukawadhihirikia na wakaanza kujibandika majani ya Peponi (humo). Na Adamu akamkosa Mola wake, na akapotea kidogo njia.” Sura 20:121 Ta Ha

Mungu alipokuja akiwatafuta wakajificha… nao wakajaribu kujifunika wenyewe kwa majani, kuficha uchi wao.
“Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo. Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone. BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini nikaogopa wa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.”
Taurati Mwanzo 3:7-10

Vazi Lifunikalo la Mungu
Katika kuchanganyikiwa kwake Adamu kwa kujikuta yu uchi, ilibidi Mungu amfunike kwa ngozi za wanyama. Ilikuwa lazima achinjwe mwana-kondoo ili kutengeneza mavazi ya mwanamume yule na mkewe ambao walikuwa uchi. Ilikuwa ni lazima damu imwagwe ili mwanadamu yule apate tena vazi lile lifunikalo. Hayo yote yalielekeza mbele kwa yule Mwana-Kondoo wa Mungu ambaye siku moja angekuja kuzichukua dhambi za ulimwengu. “…Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” Injili Yohana 1:29

Hivyo [Isa] Kristo alikuwa Kondoo wa Mungu, na ilikuwa damu yake iliyomwagika ili mwanadamu mwenye hatia aweze kusamehewa dhambi zake, na mara moja tena aipate ile haki. Mwanadamu angeweza tu kwa njia ya Yesu kuufunika tena uchi wake kwa Haki ya Masihi Isa, yaani, Yesu.
Vazi la ngozi lililowafunika lilikuwa ni la muda mfupi tu. Mwanadamu alipewa nafasi ya pili ili kuipata ile haki iliyopotea.
Lakini, basi, ni kwa jinsi gain mwanadamu angeweza tena kuipata tabia ya utakatifu iliyopotea? Mwanadamu alikuwa ameupoteza uwezo wake wa kufanya mema. Asingeweza kabisa kwa uwezo wake mwenyewe kufanya mema au kuwa mtakatifu moyoni mwake. Ni utata ulioje huo mwanadamu aliojiingiza ndani yake! Msaada ungetoka wapi?

Mungu alikuwa na mpango… katika mpango wake, angempa tena lile vazi takatifu lifunikalo. Vazi lile lingetoka kwa mwanadamu mwingine… Adamu wa pili… yaani, Kristo.

“…Nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki…” Isaya 61:10.
“Haki yako ni haki ya milele, na sheria yako ni kweli.”
Zaburi 119:142

Haki ni kitu fulani tulichokipoteza, lakini tunapomtii Mungu, na kumwamini Kristo, anatuvika tena hilo vazi. Hilo hufanyika kupitia Isa aliyeteremshwa… zingatia ya kwamba haki ni kama vazi tulilovikwa…
Ayubu, mtu mmoja kutoka miongoni mwa watu wale wa Mashariki wenye hekima kweli kweli, alisema… “Nalijivika haki, ikanifunika, adili yangu ilikuwa kama joho na kilemba.” Taurati Ayubu 29:14.”
“Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja [Adamu] mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana, wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.” Injili Warumi 5:17.”

“Ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti.” Injili 3:22

Ee mpendwa msomaji, je, utakiamini na kukipokea kipawa (zawadi) hiki cha haki kutoka kwa Mungu? Hicho ni zawadi, wala hakiwezi kupatikana kwa kufanya kazi. Vinginevyo kinakoma kuwa zawadi.

“Sio wema (tu huo peke yake) kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa Mashariki na Magharibi (katika kusali. Yako na mema mengine). Bali wema (hasa) (ni wa wale) wanaomwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu [Biblia] na Manabii…”
Sura 2.177 Al Baqarah

Tunaagizwa kuitafuta Haki. Ni dhahiri kwamba inaweza kupatikana, vinginevyo tusingeagizwa kuitafuta.

“Mtafuteni BWANA, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi, mliozitenda hukumu zake, itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya BWANA.” Sefania 2:3.”
“Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” Injili Mathayo 6:33
“Heri wenye njaa na kiu ya haki; maana hao watashibishwa.”
Injili Mathayo 5:6

Hiyo ni kwa ajili ya wote, kwa kila taifa… kwa kila mtu duniani. Ahadi zake ni za hakika.
“Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wote.” Mithali 14:34

Twaambiwa katika Kurani Tukufu ya kwamba Isa alikuwa kipawa cha mwana mwenye haki. [Sura 19:19]. “Kurani Tukufu” Alidumisha uadilifu wake mbele za Mungu na sasa akapata haki ya kutupa sisi tunaomwamini zawadi hiyo ya thamani.
Kwa hiyo ni kweli kwamba matendo mema ni matokeo ya kipawa hicho cha Haki tulichopewa. Kwa hiyo, matendo mema yanayotoka moyoni ni tunda la haki. Mara tu sisi tunapokuwa na kipawa hiki tunayo haki kamili ya kuingia Mbinguni. Hivyo yote hutegemea juu ya kukipata kipawa hiki cha Haki, kwa kweli kinafanana na vazi… nasi yatupasa kuvikwa vazi hili la mbinguni. Limefumwa katika kiwanda cha mbinguni bila kutumia ubunifu wa kidunia. Vazi hili litakupa wewe nafasi kubwa ya kuingia katika ufalme wenye Nderemoi nyingi.
“Mmoja ataniambia, kwa BWANA, peke yake, iko haki na nguvu… Isaya 45:24

Haki na sheria sikuzote huenda pamoja. Haviwezi kutenganishwa.
“Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari.” Taurati Isaya 48:18
“Ulimi wangu na uiimbe ahadi yako, maana maagizo yako yote ni ya haki.”
Zaburi 119:172
“Bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.” Injili Matendo 10:35
“…na jina lake atakaloitwa ni hili, BWANA NI HAKI YETU.”
Yeremia 23:6
Katika siku za mwisho, Wakristo wa kweli na Waislamu wa kweli wataungana na kwa pamoja watatangaza sifa za Mwenyezi Mungu na kupokea Haki yake.
“Maana kama nchi itoavyo machipuko yake kama bustani ioteshavyo vitu vilivyopandwa ndani yake; ndivyo Bwana MUNGU atakavyootesha haki na sifa mbele ya mataifa yote.” Taurati Isaya 61:11
“Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele.” Danieli 12:3
Leo hii mwombe Mwenyezi Mungu ili uweze kuwa na vazi lifunikalo la Haki ambalo linatoka kwa Isa.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana nasi:
www.salahallah.com

“Nguo za Haki”
Sehemu ya Kwanza

Sura 7:26
Al Aaraf

Mfululizo na.32

30. Nyongeza Jesus in the Quran Kiswahili

Share thisNyongeza 1.
Yesu katika Kurani: Orodha ya
Marejeo ya Kurani kumhusu Isa (Yesu)
Yesu/Isa ndiye “njia” (al sirat mustaqueem): 43:61.
Yesu/Isa ndiye “kweli” (al haq): 19:34.
Yesu/Isa ndiye “uzima” (Min Rouhina): 21:91, 66:12
Yesu/Isa:
Alizungumza na watu akiwa mtoto kitandani: 5:110, 19:24, 19:29-33.
Mimba yake ilikuwa kwa njia ya muujiza kupitia bikira aliyeitwa Mariamu na akawako kwa neno (fayakun): 3:47, 3:59, 19:20.

Mimba ilikuwa kwa uwezo wa Roho wa Mwenyezi Mungu (Rouh Al-Qudus): 21:91, 66:12.

Yeye ni Roho wa Mwenyezi Mungu (Rouh Allah): 19:17, 21:91, 66:12.
Yeye ni Roho wa/aliyetoka kwa Mwenyezi Mungu (Rouh minhu kutoka kwa Mwenyezi Mungu): 4:171.

Alitiwa nguvu/aliongozwa (ayyadhu) na Roho Mtakatifu (Rouh Qudus): 2:87, 2:253, 5:110.

Yeye na Mwenyezi Mungu wote wawili wanaitwa Bwana (rab): 9:31.
Yeye ndiye Injili au habari njema: 3:45.
Aliteremshwa (anzalata) kutoka kwa Mwenyezi Mungu: 3:53.
Aliteremshwa kutoka mbinguni (hili ni fumbo katika mapokeo ya Wasufi): 5:114-115.
Yeye ndiye Neno la Mwenyezi Mungu (kalimatu Allah): 3:39, 3:45, 4:171.
Yohana Mbatizaji anamthibitisha Yesu/Isa kuwa ndiye “Neno”: 3:39.
Mwana aliye mtakatifu, asiye na dhambi (zakiyyah): 3:46, 19:19.
Hakuwa jeuri wala mwovu: 19:32.
Hakutumia mabavu wala hakuwa mnyonge (jabbaran shakiyyan): 19:32.
Yeye ni mwenye haki (saliheen): 3:46, 6:85.
Yeye yu karibu na Mwenyezi Mungu (muqarrabeen, yaani, yuko mahali maalumu pa heshima), yeye peke yake ndiye amepewa mahali hapo katika Kurani; 3:45.

Yeye ndiye mpatanishi/mkuu/aliyetukuzwa (wajihan au wajih) sasa na hata milele. (Hii ilikuwa ni sifa ya pekee iliyotolewa tu kwa Isa na Musa, ambao kwa namna ya kuvutia sana, walikuwa ni watu wawili wanaotoa agano [ahadi]): 3:45.

Yeye ndiye mwombezi (shafa ‘a); haki ya pekee ya Mwenyezi Mungu aliyompa na kumhesabia Isa (kwa mujibu wa baadhi ya tafsiri za Wasufi): 2:255, 21:28.

Yeye ndiye njia iliyonyoka (siratun mistaqueem): 3:51, 43:61.

Amepewa siri za yale yasiyoonekana kwa macho (ghyab) (maajabu): 3:44.

Upendeleo wa Mwenyezi Mungu ulikuwa juu yake yeye: 5:110, 43:59.

Mwenyezi Mungu alimpa yeye “upendeleo” na hadhi ya nabii “zaidi ya wengine”: 2:253.

Mwenyezi Mungu alimbariki (mubarak) po pote alipokuwapo: 19:31.

Alipewa hekima na ufunuo wa Agano la Kale na Injili: 3:48, 2:36, 19:30, 43:63, 57:27.

Mwenyezi Mungu aliyadhihirisha mapenzi yake kwa Yesu/Isa: 4:163.

Mwenyezi Mungu alifanya agano [ahadi] pamoja naye: 33:7.

Yeye anafanishwa na Adamu (yeye ni Adamu wa pili): 3:59.

Aliitwa Masihi: 3:45, 4:157, 4:171, 4:172, 5:17 (mara mbili), 5:72 (mara mbili), 5:75, 9:30, 9:31.

Anakuja kuithibitisha sheria: 3:50.

Amepewa mamlaka kuhalalisha vitu vilivyoharamishwa kabla: 3:50.

Yeye ni “rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu” (rahmatun):19:21.

Alikuwa ishara dhahiri (be-yinat, yaani, “iliyo dhahiri na isiyo na shaka”) kwa watu (wanadamu wote): 2:87, 19:21, 21:91, 43:61.

Alionesha ishara dhahiri (be-yinat) za Mwenyezi Mungu: 2:253,3:49-50,5:114, 43:63.

Mwenyezi Mungu alimpa miujiza dhahiri: 2:253.

Alipewa uwezo wa kutia pumzi/kuumba uhai mpya kutoka katika udongo: 3:49, 5:110.

Aliwaponya vipofu na wenye ukoma: 3:49, 5:110.

Alikuwa na uwezo wa kuwafufua wafu: 3:49, 5:110.

Kwa muujiza anateremsha chakula duniani kutoka mbinguni. 5:112-118.

Watu walifanya hila (dhidi yake): 3:54.

Aliitwa “mwongo” halafu “wakamwua” (taqutulun): 2:8, 5:70.

Alikufa (mutawafeka kutokana na kitenzi cha Kiarabu tawwafa (kusababisha kifo) ambapo amutu shina lake ni mata (alikufa): 3:55, 4:159, 5:117, 19:33.

Alifufuliwa kutoka kwa wafu (yum uba’athu): 19:33, (yawezekana 6:122).

Alipaa kwenda kwa Mwenyezi Mungu mbinguni: 3:55, 4:158.

Anarudi siku ya kiama (yum al-qiyama): 3:55, 4:159, 43:61.

Yeye ni ishara ya na yeye anajua siku ya hukumu: 43:61.

Ni Mjumbe/Mtume (rasul): 4:157, 5:75.

Yeye ni Nabii (nabyyun) wa Mwenyezi Mungu: 19:30.

Yeye ni mtumishi (abd Allah) wa Mwenyezi Mungu: 4:172, 19:30, 43:59.

Yeye ni Shahidi (shahid) mwaminifu wa Mwenyezi Mungu: 4:159, 5:117.

Amani (salaam) i juu yake: 19:33.

Yeye ni kielelezo kwa wana wa Israeli: 43:59.

Aliwatia moyo wanafunzi (al-hawariyun) kuwa na imani kwa Mwenyezi Mungu: 5:111.

Wanafunzi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu (ansar Allah) wanaomtangaza Yesu/Isa: 3:52, 61:l4.

Wanafunzi wake wanayo mamlaka dhidi ya adui zao: 61:14.

Wanafunzi ni mashahidi wa ukweli wa Yesu/Isa: 5:113.

Sisi tunaagizwa kumtii yeye (atee’uon): 3:50, 43:63.

Tunaagizwa kumwamini yeye (aamanou): 4:159, 5:110.

Tunaagizwa kumfuata (ettabio’un) yeye: 3:55, 43:61.

Wafuasi wake wako juu (fawqua) ya wale wasioamini: 3:55.

Wafuasi wake wanakubalika (ni waumini wa kweli) (aamanou minhum) kwa Mwenyezi Mungu: 57:27.